Na Editha Karlo
Waomba hifadhi kutoka nchini Burundi wakiwasili nchini kwa boti hivi  maeneo ya Kibilizi, Mkoani Kigoma. Bado idadi yao haijafahamika kwani bado zoezi la kuwaandikisha linaelea katika eneo hilo. 
Ujio wa waomba hifadhi hawa unakuja kutokana na machafuko yanayoendelea nchini Burundi  ambayo yameshika kasi na kusababisha wananchi kuanza kukimbilia nchini Tanzania.
Burundi ilikumbwa na machafuko katika miaka ya nyuma na baadaye kuwa na amani lakini sasa inaingia katika mgogoro tena baada ya Rais wa sasa Pierre Nkurunzima kutaka kuwania urais kwa muhula mwingine.
Waomba hifadhi kutoka nchini Burundi wakijiandikisha mara baada ya kuwasili nchini Tanzania leo kwa boti.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 12 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 03, 2015

    Jamani ni huruma sana, Tanzania tuendelee na ukarimu wetu, tuwapokee tu hawa viumbe wa Mungu kwani Mungu atatulipa kwa wema wetu. Karibuni sana raia wa burundi nchini Tanzania.

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 03, 2015

    Waje tu kwetu shamba la bibi nao tutawapa uraia

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 04, 2015

    AFRIKA NI BALA LA GIZA KWELI IVI KUNA HAJA NA HAMU GANI YA KUTAKA KUENDELEA KUONGOZA ILI HALI UNAOTAKA KUWAONGOZA WAMEONESHA KUKUCHOKA AU KWA LUGHA NYEPESI BILA KUPEPESA MACHO HAWAKUTAKI, HAYA EBU ANGALIA SASA WATOTO ILIBIDI WAWE SHULE LEO WAPO KIBIRIZI, WAZEE NA AKINA MAMA NAO PIA WAPO TABUNI IVI KWELI UTAFURAIA IKULU KWA HALI HII???WAKATI MWENGINE TUNALAUMU KUHUJUMIWA NA WATU WEUPE HALI YA KUA SISI WENYEWE NDIO VIPOFU WA KUSOMA NYAKATI, ILA SITAKIWI KUSEMA SANA MAANA NASI NDIKO TUNAKOELEKEA HUKO KUNA KILA DALILI....MAANA WINGU LILILOPO SI DOGO KUACHA KUNYESHA.

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 04, 2015

    Wakati umefika jumuiya ya sfrika mashariki kuingilia na kuhakikisha amani inakuwepo kabla ya kuwa majuto badala ya kukaa kando na kupokea wakimbizi.

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 04, 2015

    Kwakuthibitisha kua sisi waafrika viongozi wetu akili zao ni zakushikiwa , kinacho tokea Burundi ndio kilekile cha uchu wa madaraka! Kiongozi anadanganywa na marafiki zake wa karibu kua wananchi wote wanakuku bali sana kwahiyo ongeza muda tena ! Matokeo yake ndio hayo ! Mkipelekwa mahakama ya kimataifa mnalalamika Mbona mahakama hii inatushughulikia sisi tu ! Waswahili wanasema Akili za kuambiwa jumlisha + na za kwako ! Hili la Burundi kunauwezekano pia likatokea Congo ! Kwa Tanzania ushauri wangu kwa wana siasa ! Tujifunze kuwa na roho ya kukinai ! Namkubari sana Mzee Mustafa Nyang'anyi . Kiongozi alie kubali kukaapembeni na kuachana na siasa bila shinikizo ! Ni heshima kubwa sana kwake mpaka kwa wananchi wake na Taifa kwa ujumla ! Viongozi wengine igeni mfano wake !

    ReplyDelete
  6. AnonymousMay 04, 2015

    IKO HAJA YA KUUNDA CHOMBO CHA AFRIKA AMBACHO KITAKUWA NA UWEZO WA KUINGILIA MAMBO YA NDANI YA KILA NCHI YA AFRIKA NA KUHAKIKISHA UPUUZI KAMA WA HUYU AITWAYE NKURUNZINZA UNAKOMESHWA NA MHUSIKA ANANAADABISHWA.

    ReplyDelete
  7. AnonymousMay 04, 2015

    Mdau wa tatu, unakosea unaposema hata sisi ndiko tunakoelekea. Hata kidogo haiwezi kutokea endapo tutasema NO. Tatizo la Tanzania kuna baadhi ya watu wachache sana wanatamani vita, ugaidi, na ukimbizi. Hili si suala la kuombea litupate. Unajua ukishabikia vita itakupata, ukishabikia umaskini utakuwa maskini mpaka mwisho. Ikulu hata siku moja haitatupa utajiri watanzania hata kiingie chama gani kama ni umaskini utabaki kuwa maskini endapo hujishughulishi. Kubwa tumwombe Mungu haya yasitupate, na pia tuwe watu wa shukrani na pongezi sio kila kitu kulaumu tu, hata Mungu hapendi hilo. Kumbuka kila mmoja hapa ni binadamu na ana makosa yake mengi tu lakini Mungu hajamuadhibu mtu, na kamwe Mungu hamuadhibu mtu tunaadhibiana sisi kwa sisi. Kwa hiyo basi, tuzidi kuomba amani itawale nchini, watakaoleta vurugu ni wale wanaong'ang'ania madaraka na kutaka kuishi Ikulu wakidhani watatatua shida za mtanzania na kumbe si hivyo. October inakuja na tutampata kiongozi tunayemtaka na baada ya mwaka mmoja hata kama atakuwa yule tuliyemuhitaji sana napo tutaanza kumlalamikia maana baadhi yetu kila wakati ni lawama tu kuliko baraka. Tusali kuomba amani itawale daima. Mungu ibariki Tanzania na watu wake.

    ReplyDelete
  8. AnonymousMay 04, 2015

    African Union has to assume more responsibility;esp.that of unseating of despots.In fact they are fashionably becoming too much of a crowd.AAARG !!!!

    ReplyDelete
  9. Au ni mpango wa muda mrefu kuhamia Tanzania? Viongozi wa Burundi nwanaanzisha vurugu makusudi huku wakijua wananchi wao watapokelewa Tanzania na hatimaye kupewa uraia. Matatizo ya ardhi ndogo na uchumi mbaya yanapungua.

    ReplyDelete
  10. AnonymousMay 04, 2015

    Jamani jamani wannchi mbona wanahangaihwa na mambo ya uchaguzi kiasi hiki. Afrika tunahitaji kozi ya kufanya chaguzi za amani.

    ReplyDelete
  11. AnonymousMay 04, 2015

    Viongozi wa nchi hizi za kiafrica wako si kwaajiri ya wananchi bali kwa mambo yao binafsi.Cha kushangaza wanalindana....Kumbuka ni viongozi hao hao waliopinga kwa nguvu swala la kutompeleka Rais Kenyatta kwenye mahakama ya kimataifa lakini wale wananchi walio athiliwa na machafuko yale awaogelewi kabisa,sasa linakuja tena la Burundi.Ni shiidaaa

    ReplyDelete
  12. AnonymousMay 04, 2015

    Mh Kikwete pamoja na washauri wako wa nchi hii nakuomba Rais wangu tumia nguvu zako zote ulizonazo kutatua tatizo la Burundi.

    Ni Juzi juzi tu nimetoka ku-comment hapa hapa kwamba kama JK hautoingilia kati ili swala basi matatizo yatakuwa kwetu Sisi Watanzania kwa 1: wimbi la wakimbizi 2: Silaha nyingi kuingia nchini 3: Ujambazi utaongezeka, nk

    Mh JK nakuomba nenda moja kwa moja Burundi bila ya kumtuma mtu yoyote au kumuogopa huyu Pierre Nkurunziza na muweke sawa na mwambie wazi huyo Bw mdogo kwamba tumemchoka!!

    Inabidi Tanzania ioneshe nguvu yetu na Ukubwa wetu na uwezo wetu wa kutoa kauri kama Taifa lenye nguvu Afrika! Tukitaka tuheshimike duniani na Afrika inabidi tuoneshe thamani yetu na ndio maana unaona nchi kama US na Russia zimekuwa Super Power duniani kwa Uwezo wao wa kuweka Order duniani na Sisi Kama Tanzania inabidi tuoneshe nguvu zetu kwa kuweka Order ndani ya EA na kuendelea pole pole hadi Afrika nzima...Tuache maswala ya kuogopana na kuoneana haya wakati watu wanakufa ndani ya Burundi na Tanzania itakuja kupata madhara baadae, Mauaji ya Rwanda na Burundi yalikuwa hivi hivi kwa kosa la kushindwa ku-act mapema!!

    Pierre Nkurunziza ni nani haswa Afrika nzima iweze kumuogopa na kushindwa kumwambia wazi wazi kwa kauri ya wazi wazi kwamba haondoke madarakani??!! You cannot involve diplomacy with somebody who cannot respect and obey Democracy and Constitution of her Country!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...