Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Prof Makame Mbarawa (watatu kushoto mstari wa nyuma) akishuhudia utiaji saini wa mikataba ya mradi wa mawasiliano vijijini Awamu ya 2B ambapo makampuni ya simu ya TTCL, Vodacom na Tigo walisaini. Wanaosaini kutoka kushoto ni Afisa Mtendaji Mkuu wa TTCL, Dk. Kamugisha Kazaura, Afisa Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Mawasiliano Injinia Peter Ulanga, Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano wa Vodacom,Rosalynn Mworia na Mwakilishi wa kampuni ya MIC, Slyvia Balwire. Sherehe hiyo ilifanyika mkoani Dodoma jana.
Afisa Mkuu Mtendaji wa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote, Injia Peter Ulanga akibadilishana hati za makubaliano na Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano wa Vodacom Tanzania Rosalynn Mworia mara baada ya kusaini mkataba wa kupeleka mawasiliano ya simu vijijini, katika sherehe zilizofanyika mjini Dodoma leo.

Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Prof Makame Mbarawa (katikati) akiwa na Wawakilishi wa makampuni ya simu yaliyosaini mkataba wa kupeleka mawasiliano ya simu vijijini sherehe iliyofanyika mjini Dodoma jana. Wengine ni Mwakilishi wa Bodi ya Mfuko wa Mawasiliano, Aumsuri Moshi (kushoto) na Afisa Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Mawasiliano Injinia Peter Ulanga. Mstari wa nyuma ni wawakilishi wa makampuni hayo ya simu, Afisa Mtendaji Mkuu wa TTCL, Dk Kamugisha Kazaura, Mwakilishi wa Vodacom Tanzania, Rosaline Mworia na Mwakilishi wa MIC Tanzania Ltd, Sylivia Balwire.

Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia,Prof Makame Mbarawa,(pili kushoto) akiwa na Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano wa Vodacom Tanzania Rosalynn Mworia mara baada ya kampuni ya Vodacom kuwa kati ya makampuni matatu yaliyo saini mkataba wa kupeleka huduma ya mawasiliano simu vijijini awamu ya 2B katika sherehe zilizofanyika mjini Dodoma leo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...