Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Kamishna wa Polisi (CP) Diwani  Athumani Msuya (pichani kushoto) , kuwa Mkurugenzi wa Upelelezi wa makosa ya Jinai (Director of Criminal Investigation).

Kabla ya uteuzi huu CP Msuya alikuwa Kaimu Kamishna wa kamisheni ya Intelijensia ya Jinai. CP Msuya anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Ndugu Robert S. Manumba ambaye amestaafu kwa mujibu wa Sheria.

Rais Kikwete pia amemteua Naibu Kamishna wa Polisi (DCP) Valentino Mlowola (kulia) kuongoza Idara ya Intelijensia ya Jinai, kujaza nafasi inayoachwa na Kamishna Msuya.

Kabla ya Uteuzi huu, DCP Mlowola alikuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza.

Uteuzi huu umeanza tarehe 3 Mei, 2015

Imetolewa na; 

Premi Kibanga,
Mwandishi wa Habari wa Rais Msaidizi,
Ikulu – Dar es Salaam.
12 Mei, 2015.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 12, 2015

    Napenda kuwashauri Kurugenzi ya Mawasiliano Ikulu maana naona mna google mail a/c kwanini msiombe nchi nyingine rafiki wawatengenezee Secure Network muwe mnatumia secured Communications? Au pia kwanini msiombe Idara ya Usalama wa Taifa wawasaidie kufanikisha ili?

    Kwanini nasema hivyo?

    1: Mataifa mengine yasiyo rafiki yanaweza kufahamu kila kitu mnachowasiliana kwa kuweza kuhack hiyo a/c ambayo ni very easy.

    2: Google wenyewe sio wa kuwaamini kabisa maaana wana Systems ambazo pia utuma moja kwa moja NSA na Idara nyinginezo na kufanya mambo yetu kujulikana. Hii ni kwa kila Kampuni binafsi za email.

    3:Virus and trojans ni rahisi sana kuwa planted through phishing emails.

    4: Mawasiliano yenu uenda yakawa sio Muhimu kama mnavyodhani ila ni rahisi sana kwa kutumia trojans and virus kwenda ktk hiyo email na kutumika kama njia ya kuwezesha kufika sehemu nyeti zaidi.

    5: Mwisho ningeomba msitishe kutumia email za makampuni binafsi na muanza mchakato wa kuweza kuwekeza kwenye kutengeneza Mtandao ambao secure kwa mawasiliano yenu na kwa Taifa.

    Mifano hii ipo wazi ata kwa mataifa mengine ambapo juzi tu White house ilikuwa hacked kwa uzembe kama huu tu hachilia mbali Mrs Hillary Clinton alivyopata majanga kwa kutumia email binafsi kama hiyo badala ya kutumia secure Connection kwa mawasiliano ya Kitaifa, nk

    Nimeamua kuweka wazi kwakuwa mimi ni Mtanzania ninayependa nchi yangu sana sana na mwenye elimu hii. Asante

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 12, 2015

    Nadhani Habari haiko sawa hivi muda wote huo kamishna Manumba aondoke DCI Mungulu alikuwa akifanya kazi gani

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...