Waziri wa Elimu na mafunzo ya ufundi Dkt.Shukuru Kawambwa akimkaribisha Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete katika uwanja wa michezo wa Jamhuri mjini Dodoma  kuongoza sherehe za kilele cha wiki ya Elimu kitaifa Mei 15,2015. 
 Balozi wa Chini nchini Tanzania,Lu Youging akizungumza jambo na Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete katika uwanja wa michezo wa Jamhuri mjini Dodoma  kuongoza sherehe za kilele cha wiki ya Elimu kitaifa Mei 15,2015,kulia ni Naibu Waziri wa Elimu na mafunzo ya ufundi Mh.Anne Kilango Mallecela. 
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimpa zawadi mwanafunzi Agatha Julius Ninga kutoka Shule ya sekondari ya wasichana ya Tabora akiwa ni miongoni mwa wanafunzi sita waliofaulu vizuri katika mitihani ya sayansi ya kidato cha nne mwaka jana 2014.Agatha alifanya vizuri katika somo la Biolojia.Rais Kikwete alitoa zawadi kwa wanafunzi, shule,halmashauri na mikoa iliyofanya vizuri na kuongeza ufaulu katika mitihani ya Taifa kumaliza Elimu ya msingi na elimu ya sekondari.Tuzo na zawadi hizo zilitolewa leo katika uwanja wa michezo wa Jamhuri mjini Dodoma wakati wa maadhimisho ya kilele cha wiki ya elimu nchini.
Waziri wa Elimu Dkt.Shukuru Kawambwa akitoa tuzo maalum kwa Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete kwa kutambua mchango wake katika kuendeleza na kuboresha elimu nchini wakati wa maadhimisho ya kilele cha wiki ya elimu yaliyofanyika katika uwanja wa michezo wa Jamhuri mjini Dodoma leo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...