Ofisa Uhusiano na Uhamasishaji wa Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA), Fulgence Sebera akimpatia zawadi Naibu Waziri wa Kazi na Ajira, Dk. Makongoro Mahanga, wakati alipotembelea banda la mamlaka hiyo katika maonesho hayo, mjini Dodoma, yaliyofanyika kuanzia 26 - 28 April 2015.
Ofisa Mwandamizi wa Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA), Utawala na Rasilimaliwatu, Amina Ally (kushoto) akimuaga Naibu Waziri wa Kazi na Ajira, Dk. Makongoro Mahanga, wakati alipotembelea banda la mamlaka hiyo katika maonesho ya Siku ya Usalama na Afya mahala pa kazi mjini Dodoma, iliyofanyika kuanzia 26 - 28 April 2015.Katikati ni Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Mh. Betty Mkwasa.
Katibu Mkuu wa Shirikisho la Vyama Huru vya Wafanyakazi nchini (TUCTA), Nicholas Mgaya (kushoto), akisalimiana na Maofisa wa Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA), mjini Dodoma, wakati wa maonesho hayo yaliyofanyika kuanzia 26 - 28 Aprili 2015.
Ofisa Mwandamizi wa SSRA, Utawala na Rasilimali watu, Amina Ally, akiwahudumia wananchi waliofika kwenye banda hilo la Mamlaka hiyo, katika maonesho hayo, mjini Dodoma.
Maofisa wa Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA), wakiwa kwenye maonesho hayo kwa ajili ya kuwapatia wananchi huduma mbalimbali zitolewazo na mamlaka hiyo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...