Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) imewasii salama leo alfajiri ikitokea nchini Afrika Kusini ilipokua ikishiriki michuano ya Kombe la Cosafa, baada ya kutolewa katika hatu ya awali ya makundi.

Stars ambayo jana jioni ilipoteza mchezo wake wa mwisho dhidi ya Lesotho baada ya kufungwa bao 1 - 0, imerejea baadaa ya kupoteza michezo yote mitatu ya kundi B, baada ya kufungwa na Swaziland, Madagascar na Lesotho.

Mara baada ya mchezo wa jana dhidi ya Lesotho, kocha mkuu wa Taifa Stars Mart Nooij alisema amesikitishwa na matokeo ya timu yake katika hatua hiyo ya awali baada ya kupoteza michezo yote mitatu.

Nooij alisema, mpira wa miguu umebadilika kwani matarajio yake yamekua tofauti, kwani kiwango walivyoonyesha wapinzani wake katika kundi B vimemstajaabisha.


“Mpira wa sasa hautazami nani yupo juu katika renki za FIFA, tulikua na matarajio ya kufanya vizuri katika michuano hii lakini baada ya dakika ya 90 za kila mchezo matokeo hayakua mazuri kwetu” alisema Nooij”


Kuhusu kufuzu kwa AFCON 2017, Nooij amesema katika kikosi chake alichokwenda nacho Cosafa alikua na wachezaji saba aliowapandisha, anaamini wamepata uzoefu, na sasa atawajumuisha na wachezaji ambao hawakuweza kushiriki michuano hiyo kujiandaa na mchezo dhidi ya Misri.

Taifa Stars inatarajia kucheza kucheza mchezo wake wa kwanza wa kuwania kufuzu kwa AFCON 2017 dhidi ya Misri, tarehe 14 Juni 2015 katika uwanja wa Borg el Arab jijini Alexandria.

IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 23, 2015

    Huyu kocha hovyo, raking za FIFA kwani Tanzania ipo ya ngapi? Nchi zote zilizoshinda zipo juu ya Tanzania.

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 23, 2015

    Kauli ya kuhusu ranking ingefaa kutolewa baada ya timu yetu kuzifunga timu zilizo juu yetu.

    ReplyDelete
  3. Afukuzwe bwege tu

    ReplyDelete
  4. Inawezekana tatizo likawa kwa kocha ila nijuavyo mimi na watanzania wengine wenye ujuzi wa mpira wa kibongo ni kwamba, wachezaji wetu wa Taifa Stars wengi si wachezaji kweli, wale ni wana mazingaombwe tu. Mpira siku zote unatokana na kipaji cha mtu si uchawi kama tufanyavyo sisi. Wachezaji wa kibongo wanaroga mpaka kocha wa Taifa? Ebu angalia kwa mfano mtu kama Ngassa ana mpira gani, kisha Ngassa huyo huyo anatwakilisha watanzania kama si ujinga ni nini? Kwa mtizamo huu tutaendelea kufungwa milele tena hata na vibonde Djibouti.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...