Mkurugenzi wa  Idara ya  Masuala ya Sheria,  Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa,  Balozi Irene Kasyanju akiwa na Kanali, Dkt. Edward Masalla kutoka Jeshi wa  Wananchi wa Tanzania ( JWTZ) na Afika Mkuu wa  Uwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa Bw. Abdalla Khamis,  timu hii  ndiyo iliyoiwakilisha  Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  katika  mkutano wa Marejeo wa Mkataba wa  Silaha za Nyukilia  (NP 2015) mkutano huu  ambao kwa kawaida hufanyika kwa wiki nne umemalizika pasipo wajumbe kufikia mabakubaliano ya pamoja ya baadhi ya   vipengere muhimu.
 Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa,  Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa  Kimataifa,  Balozi  Celestine Mushy katika mkutano   uliokuwa  ukijadili  ajenda ya tathmini na ufuatiliaji wa  utekelezaji wa ajenda na malengo ya maendeleo endelevu baada ya 2013  mkutano  ambao pia  ulipitisha mada zitakazojadiliwa wakati wa Mkutano Kisiasa wa Ngazi ya Juu wa Viongozi Wakuu wa Nchi na Serikali watakapokutana mwezi septemba  ambapo  wanatarajiwa kupitisha ajenda na malengo ya maendeleo endelevu baada ya 2015. Aliyeketi  nyuma ya Balozi Mushy  ni Dkt. Tausi Kida  Mkurugenzi Mtendaji  wa  ESRF. Anayeonekana nyuma kabisa ni  Bw.  S. Shilla Afisa Mkuu wa Uwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa.
 
 Ujumbe wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  ulioshirikia majadiliano kuhusu tathmini na ufuatiliaji wa utekelezaji wa  malengo ya maendeleo endelevu  baada ya 2015 kutoka kushoto ni  Bw. Ahmed Makame Haji, kutoka Tume ya Mipango Zanzibar,  Bi. Salma Ali Kimara   Tume ya  Mipango Zanzibar na Bw. Senya Robert Tuni kutoka  Tume ya Mipango Tanzania Bara.
Sehemu ya  wajumbe wa  Nchi wanachama  zilizoshiriki katika mkutano wa  Majadiliano kuhusu eneo la  tathmini na ufuatiliaji wa  utekelezaji wa  ajenda  na malengo ya maendeleo  endelevu baada ya 2015. Mkutano huo   wa wiki moja umemalizika  mwishoni wa  juma hapa makao makuu ya umoja wa mataifa.

Jaji Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Othman Chande ambaye yupo hapa Umoja wa Mataifa  kwa kazi maalum akiwa  na Kutoka kulia,  Mkurugenzi wa DMC. Balozi Celestine Mushy,   Dr. Tausi Akida na Mdau Kutoka Idara ya Siasa ya Umoja wa Mataifa. 



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...