Katibu Mkuu wa Umoja wa Madereva nchini, Rashid Saleh akizungumza na baadhi ya Madereva wenzake walioingia kwenye mgomo leo, kuishinikiza Serikali kuwatimizia matakwa yao waliyoyaomba kwa kipindi kirefu kilichopita.
Sehemu ya Umati wa Madereva hao ukimsikiliza kiongozi wao, mchana wa leo kwenye Stendi kuu ya Mabasi, Ubungo jijini Dar es salaam.
 Taswira ya kituo cha Simu 2000 Ubungo jijini Dar es Salaam leo baada ya mgomo wa madereva wa mabasi ya abiria.Picha zote na Avila Kakingo,Globu ya Jamii.
 Barabara ya Sam Nujoma eneo la Ubungo jijini Dar es Salaam leo.
 Licha ya mgomo wa madareva Miundombinu ya maji machafu hakuna katika kituo cha Mabasi Yaendayo mikoani cha Ubungo jijini Dar es Salaam.
Hakuna kukanyaga maji ni kuruka mawe tuu.
 Mabasi yakiwa yameegeshwa katika Stendi kuu ya Mabasi yaendayo mikoani-Ubungo jijini Dar es Salaam leo.

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 8 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 04, 2015

    Halafu kila siku mnasema turudi tanzania!!..dah maisha magumu sana..hebu ona uchafu uchafuuu maji taka kila mahali..wizi,ufisadi,ujangili!

    uncle eeh njoo mamtoni umalizie miaka yako ya kuishi angalau uenjoy kabla hujafa mtu wangu!

    mdau
    Washington DC

    ReplyDelete
    Replies
    1. AnonymousMay 05, 2015

      Acha uzushi wewe, sisi tunakufahamu. Kazi yako unalinda wazee na watu wasiojiweza huko mamtoni, halafu unajitia una wakoga wenzako. Wabongo bana! Kuishi Marekani, yeye anajiona wa maana.

      Delete
  2. AnonymousMay 04, 2015

    Walau ajali zimepungua leo kwa mgomo huu. Maana hata trafiki wanachangia sana ajali.

    ReplyDelete
  3. Leteni mbinu za kutatua changamoto wadau kuliko kuponda kwenu. Kwenu ni kwenu tu hata iweje

    ReplyDelete
  4. Mdau hapo juu anaponda nchi yake hahaha so ughaibuni mbona nako kawaida tu

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 05, 2015

    Mie namkaribisha uncle Scandinavia kwa utulivu zaidi achana na Ma Dc hakuna tofauti na bongo......

    ReplyDelete
    Replies
    1. AnonymousMay 05, 2015

      Mzushi mwingine huyo, Scandinavia kuna kitu gani, kijijini huko? Marekani bado iko juu tu, ila alichokosea huyo mdau ni kuponda kwao. Ni kweli kama alivyosema msemakweli watu walio ughaibuni wanatakiwa kuchangia kwa kiasi kikubwa maendeleo kwenye nchi yao. Ila kuna shida ya baadhi ya watendaji wa Serikali kuendekeza urasimu kwa wanaohitaji kuwekeza nyumbani.

      Delete
  6. TWILA KAMBANGWAMay 05, 2015

    alafu huyo jamaa huko marekani hata kibali cha kuishi huko hana, anaishi kwa kujifichaficha tu, na anashindwa hata kwenda kutembelea ndugu home tanzania, ukimuuliza una muda gani hujenda home? atakwambia miaka 13 kumbe hana hati ya kusafiria huyo bwege.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...