Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini TFF, leo hii imekubali kuwa wenyeji wa michuano ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati ngazi ya Vilabu maarufu kama CECAFA Kagame Cup.
CECAFA ambao ndio wamiliki wa mashindano haya watatoa mialiko kwa vilabu vyenye sifa ya kushiriki na wakipokea uthibitisho wa ushiriki wao watatoa orodha ya vilabu shiriki na ratiba ya michuano hiyo.
Michuano hii inatarajiwa kuafanyika nchini kuanzia tarehe 11 Julai mpaka 02 Agosti 2015.
IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...