Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii.

VYAMA vya Siasa nchini katika kuelekea Uchaguzi Mkuu vimetakiwa katika ilani zao, kuweka vipengele vya watoto kutokana na kuwepo kwa sheria kandamizi dhidi ya mtoto.

Hayo wameyasema watoto wakati wa mkutano uliondaliwa na Shirika la Save the Children kupitia Ajenda ya Mtoto inayoshirikisha mashirika 30 yanayojighulisha na masuala ya watoto kwa kuwakutanisha viongozi wa vyama vya siasa na watoto ,katika kujadili nafasi ya mtoto katika ilani zao kuelekea uchaguzi mkuu uliofanyika katika Heteli ya Kebbys,jijini Dar es Salaam leo.

Mwakilishi wa Baraza la watoto la Wilaya ya Arusha Mjini,Omary Hassan amesema sheria kandamizi ya mtoto ni ya ndoa ambayo inasema mtoto wa miaka 14 anaweza kuolewa iwapo wazazi wataridhia wakati sheria hiyo inasema mtoto ni yule aliye chini ya miaka 18.

Amesema vyama vya siasa vinawajibu katika ilani zao kuweka masuala ya watoto kutokana na vyama kila vikiingia katika uchaguzi huwa havina vipengele katika ilani zao za uchaguzi vinavyolenga watoto.

Katibu Mwenezi wa Chama cha Ukombozi na Maendeleo(CHAUMA ),Eugin Kabendela amesema katika ilani za vyama kuelekea uchaguzi kuweka vipengele vya watoto vitakavyosaidia katika serikali ijayo kutoa msukumo katika masuala mbalimbali ya watoto.
Mwakilishi wa Idara ya habari na Mawasiliano wa shirika linalo shughulikia mambo ya watoto la  Save the Children, Ellen Otaru akizungumza wakati wa kufungua mkutano wa watoto  uliowakutanisha  baadhi ya viongozi wa vyama vya siasa ,katika  mkutano uliofanyika katika Hoteli ya Kebbys jijini Dar es Salaam leo.
 Meneja Mkuu wa shirika  linalo shughulikia mambo ya watoto la  Save the Children Musa Mgata akizungumza na wadau mbalimbali wa siasa hawapo pichani,  waliohudhuria katika mkutano na watoto uliofanyika katika hoteli ya Kebbys jijini Dar es Salaam leo.
Mjumbe Mwakilishi na wanahabari wa Baraza la la watoto wa Temeke Maria Miraji akitoa maada mbele ya wadau mbalimbali katika mkutano wa watoto uliofanyika katika hoteli ya Kebbys jijini Dar es Salaam leo.
 Picha ya Pamoja ya watoto na  baadhi ya viongozi wa vyama vya Siasa wakiwa nje hoteli ya Kebbys jijini Dar es Salaam leo.Picha na Avila Kakingo,Globu ya Jamii.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...