Watu watatu wamepoteza maisha leo baada ya basi la abiria  liitwalo Super Feo linalofanya safari zake toka Mbeya Songea baaya ya kupata ajali maeneo ya Inyara mkoani Mbeya likiwa na abiria 20. 
Habari zinasema dereva wa basi hilo lenye uwezo  wa kubeba abiria 53 kutaka kulipita gari lingine  bila ya uangalifu ambapo akakutana na roli mbele yake hivyo katika kujiokoa akakimblia kulia zaidi ndipo basi likapinduka mara tatu na kufikia kwenye kalvati.
Waliotajwa kupoteza maisha ni Anastazia Ngonyani, Robert Lyman kutoka  Marekani na mwanaume ambaye bado hajafahamika jina.
Abiria 13  wako salama dereva wa basi anaitwa shafii ngaiyo ametoroka baada ya tukio.
Taarifa zinasema watu kadhaa wamejeruhiwa ikiwa ni pamoja na Patriki Mwimbila dereva msaidizi wa basi hilo ambaye amevunjika mguu. 
Majeruhi wengine waliotajwa na ambao wote wamelazwa katika hospitali ya rufaa ya Mbeya ni Sakeni mwandanege, Fatuma nyambi na Feliciana mwalongo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...