Makamu wa Rais wa Acacia, Deo Mwanyika (wa pili kushoto waliokaa) akitiliana saini ya
Makubaliano na wawakilishi wa halmashauri za Wilaya ya Msalala na halmashauri ya Mji wa
Kahama. Wa kwanza kulia ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Msalala, Patrick Karangwa
anaemfuatia ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Kahama, Felix Kimaryo. Wanaoshuhudia
ni Kamishna Msaidizi wa Madini- Ukaguzi wa Migodi, Ally Samaje (wa kwanza kulia
waliosimama) na Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Benson Mpesya (wa tatu kutoka kulia-
waliosimama).
Makamu wa Rais wa Acacia, Deo Mwanyika (wa pili kushoto waliokaa) akitiliana saini ya
Makubaliano (MoU) na wawakilishi wa Halmashauri ya wilaya ya Tarime. Wa kwanza kulia ni
Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Tarime, Jeremiah Minja akifuatiwa na Mwenyekiti wa
halmashauri ya Tarime, Amos Sagara. Wanaoshuhudia ni Kamishna Msaidizi wa Madini- Ukaguzi
wa Migodi, Ally Samaje (wa kwanza kulia waliosimama) akifuatiwa na Mweka hazina wa
halmashauri hiyo, Julius Ndyanabo (mwenye shati jeupe).
Kamishna Msaidizi wa Madini- Ukaguzi wa Migodi, Ally Samaje akifafanua jambo kabla ya tukio
la utiaji saini ya Makubaliano (MoU) ya ulipaji wa ushuru wa huduma (Service Levy) baina ya
Kampuni ya Acacia Mining Limited na halmashauri za wilaya ya Tarime, Kahama na Msalala
lililofanyika tarehe 10 mwezi Juni mwaka huu.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...