Meneja Huduma kwa Jamii wa Airtel Tanzania, Hawa Bayumi (wa pili kulia ), akimkabidhi zawadi ya mashine ya kushonea 'cherehani', kwa Betha Benedict (wa pili kushoto), mkazi wa Bunju Jijini Dar es Salaam baada ya kuwezeshwa na mpango wa Airtel Fursa “Tunakwezesha”. Kushoto ni mama yake Betha na kulia ni Meneja wa Airtel, Fadhili Mwasijeba.
Bertha Benedict (watatu Kulia) akionyeshwa na meneja Huduma wa jamii wa Airtel Hawa Bayumi (wapili Kulia) vifaa alivyokabidhi na Airtel kupitia mpango wake wa Airtel Fursa. Kushoto ni   Irene Paul balozi wa Airtel kupitia mpango wa Airtel Fursa,  mama yake Betha na kulia ni Meneja mauzo wa Airtel kanda ya kusini, Fadhili Mwasijeba.
 Bertha Benedict (Kulia) akisalimiana na viongozi mbalimbali wa Airtel mara baada ya kuwasili nyumbani kwake kwaajili ya kukabidhi zawadi kupitia mpango wa Airtel Fursa  (katikati), Meneja Huduma kwa jamii wa Airtel Tanzania Hawa Bayumi.
Wafanyakazi wa Airtel wakishusha zawadi  zilizokabidhiwa kwa Bertha Benedict (hayupo pichani)  mkazi wa Bunju Jijini Dar es Salaam baada ya kuwezeshwa na mpango wa Airtel Fursa “Tunakuwezesha”.
Wafanyakazi  wa Airtel wakiwa katika picha ya pamoja na Bertha Benedict (wapili Kulia) mara baada ya kuwezeshwa na Airtel kupitia mpango wake wa Airtel Fursa. Kutoka kushoto ni Irene Paul balozi wa Airtel kupitia mpango wake wa Airtel Fursa, mama yake Bertha, Hawa Bayumi na Meneja mauzo wa Airtel  kanda ya kusini , Fadhili Mwasijeba


KAMPUNI  ya Simu za Mkononi ya Airtel Tanzania kupitia mpango wake wa Airtel Fursa ambao umelenga kuwawezesha vijana wajasiliamali wadogo wadogo nchini umetoa msaada mwingine tena jijini Dar es salaam kwa msichana mjasiriamali Bertha Benedicto.

Bertha ambaye amelelewa katika Kituo cha Kulea watoto cha Dogodogo Center Kilichopo Bunju Jijini Dar es Salaam na kuhitimu mafunzo ya mwaka mmoja ya ufundi wa kushona nguo kituoni hapo amepatiwa vifaa mbalimbali pamoja na cherehani ya kisasa ili kuendeleza ujuzi wake.

Akiongea wakati wa makabithiano Meneja wa mahusiano ya jamii wa Airtel Bi Hawa Bayumi alisema  “ Airtel tumeona ni vyema kupitia mpango wetu wa Airtel Fursa kumpatia vifaa na mashine hii ya kisasa ya kushonea Bi Bertha Benedecto  kwa lengo la kumwezesha kuendesha shughuli zake za kiuchumi kwa ufanisi zaidi.  Sambamba na hilo  tumeweza kumpeleka kwenye mafunzo ya kumsaidia  kujijenga, kuweka mahesabu yake na kuendesha biashara yake ili aweze kukuza biashara na kuisaidia familia yake”.

Tunaamini hii ni nafasi ya pekee kwa vijana wadogo kati ya umri wa miaka 17 mpaka 24 walioko katika maeneo mbalimbali ya nchi kuweza kufaidika na mpango huu wa Airtel Fursa wenye lengo la kuwawezesha vijana wajasiriamali wadogo wadogo kukuza mitaji na biashara zao kwa ujumla. Aliongeza Bayumi”

Akizungumza mara baada ya kupokea msaada huo, Bertha amesema vifaa hivyo vitamwezesha kuendesha maisha yake na familia kwa ujumla huku Mama yake Immaculate Makinda akiishukuru Airtel kwa kuwa mkombozi kwao.

Bertha alisema, “nawashukuru sana Airtel kwa kuweza kufanikisha ndoto zangu. Kwa kuweza kunipatia vifaa hivi vya kisasa. Nimekuwa nikipata ugumu wa kupata wateja kwani sikuwa na vitendea kazi vya kutosha vitakavyoweza kukidhi mahitaji ya wateja wangu lakini sasa naamini nitapata wateja wengi sana na kuinua biashara yangu”

Kwa upande wake Mratibu wa Dogodogo Centre, bw.Issa Buzohela alisema, anaiomba kampuni ya Simu ya Airtel  kuendelea kukisaidia kituo hicho na kuinua vipaji vya vijana kwani nchi yetu imezungukwa na vijana wenye vipaji mbalimbali lakini hawana uwezo wa kuendeleza vipaji vyao.

Mpaka sasa Airtel Fursa  imeshawawezesha vijana mbalimbali na kuboresha shughuli zao za kiuchumi kwa kuwapatia vitendea kazi  na kuwaingiza katika warsha za mfunzo ya Airtel Fursa ili waweze kutimiza ndoto zao.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...