Baadhi ya wateja wa Benki ya CBA Tanzania wakipakua chakula cha futari iliyoandaliwa kwa ajili yao kwenye hoteli ya serena mwishoni mwa wiki
 Wateja wa Benki ya CBA Tanzania wakipata futari iliyoandaliwa na benki hiyo kwa ajili yao kwenye Hoteli ya Serena Mwishoni mwa wiki.
 Mkurugenzi wa Benki ya CBA Tanzania Julius Mcharo akiongea na wateja na wafanyakazi wa benki hiyo waliohudhuria futari iliyoandaliwa na benki hiyo kwenye hoteli ya Serena mwisoni mwa wiki.


.MkurugenzI na Maofisa waandamizi wa benki hiyo katika picha ya pamoja baada ya futari hiyo
 *********
Benki ya CBA Tanzania leo imewafuturisha baadhi ya wateja wake wa jijini Dar es Salaam ikiwa ni sehemu ya kuboresha uhusiano na wateja  ambapo pia itawaandalia wateja wake futari kwenye maeneo mbalimbali iliko na matawi nchini .


Akizungumza wakati wa futari iliyoandaliwa na CBA Tanzania kwa wateja katika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam,Mkurugenzi Mkuu wa benki hiyo Bw.Julius Mcharo alisema “ Tunawashukuru sana wateja wetu nchini kote kwa kuendelea kuiamini benki yetu katika kupata bidhaa na huduma za kibenki na ndio maana tunashirikiana nao sana katika maeneo maalum ambayo yanatukutanisha ili pia tuweze kujadiliana na kuboresha ushirika wetu kama tunavyokutana leo kwenye futari hii”.


Alisema Benki ya CBA Tanzania huwa inakutana na kushirikiana na wateja wake katika masuala mbali mbali ya jamii ikiwemo michezo burudani na hata katika matukio ya kuchangia kuinua sekta mbali mbali mfano afya na elimu. “Lakini leo ni siku muhimu kwetu hapa Dar es Salaam kwa kuwa tunafuturu pamoja na kutakiana mfungo mwema wa mwezi wa Ramadhani  ambao unaendelea”.


Bw.Mcharo aliahidi kuwa Benki itaendelea kuboresha bidhaa na huduma zake ili ziendelee kuwa na ubora wa hali ya juu kabisa ikiwa ni pamoja na kubuni huduma mbalimbali za kuwarahishia maisha wateja wanapohitaji kupata huduma za kibenki na kuboresha shughuli zao.

“Benki ya CBA Tanzania tunawatakia mfungo mwema wa Ramadhani lakini pia maandalizi mema ya sikukuu!, endeleeeni kufurahia huduma zetu mbalimbali na msiache kutembelea  matawi yetu au kutembelea mtandao wetu kwa njia ya kisasa ya  kuona huduma zetu mbalimbali kama vile huduma ya mkopo wa bima ambayo inaonekana kuwa mkombozi kwa watu wengi,mikopo ya kununua nyumba yenye masharti nafuu pia tunatoa huduma ya M-Pawa kwa kushirikiana na Vodacom inayowezesha wateja wa M-Pesa kuweka akiba na kupata mikopo kwa haraka na bila masharti magumu.” Alisema
Benki ya CBA Tanzania imekuwa mstari wa mbele katika kusaidia uboreshaji wa maisha ya jamii kwa kutoa misaada ya aina mbalimbali na kudhamini shughuli za miradi ya maendeleo.Bado CBA ina mpango wa kutoa misaada katika mikoa ya mbalimbali kwa dhumuni la kuendelea kupunguza tatizo la kipato kwa wananchi wanaoishi katika mazingira magumu.

CBA Tanzania ni sehemu ya CBA Group iliyopo katika nchi za Kenya, Uganda na Tanzania, CBA Tanzania ina matawi kumi na moja, iko katika mikoa ya mwanza, Moshi, Arusha, Mtwara, Mbeya na Tunduma.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...