MUFTI  Mkuu wa Tanzania, 
Sheikh Issa Bin Shaaban Simba, 
enzi za uhai wake.

Habari zilizofika chumba chetu cha habari mapema asubuhi leo na kuthibitishwa na mamlaka husika zinasema Mufti Mkuu wa Tanzania,  Sheikh Issa Bin Shaaban Simba,  amefariki dunia alfajiri ya leo katika hospitali ya TMJ jijini Dar es Salaam. 


Habari hizo zinasema mwili wa marehemu umeondolewa hospitali hapo na kuhamishiwa hospitali kuu ya Jeshi ya Lugalo kungoja taratibu za mazishi.

  Kwamujibu Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Mussa Salum
 amesema kuwa marehemu alikuwa akisumbuliwa na maradhi ya moyo pamoja na presha.
Mwili wa marehemu utasafirishwa kesho mkoani Shinyanga  kwaajili ya maziko.
  Tutaendelea kuwaletea taarifa zaidi 
kwa kadri  zitapopatikana.


Inna lillahi wa inna ilayhi raji'un 
إِنَّا للهِ وَإِنَّـا إِلَيْهِ رَاجِعونَ‎) 

Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Mheshimiwa Dkt. Fenella Mukangara (Mb.) ametuma salamu za rambirambi kwa Baraza Kuu la Waislamu Nchini (BAKWATA) na Waislamu wote nchini kufuatia kifo cha Sheikh Mkuu wa Tanzania Mufti Shaaban Issa Bin Simba kilichotokea Jumatatu, tarehe Juni 15,2015 katika hospitali ya TMJ Jijini Dar es Salaam alipokuwa anatibiwa.

Katika salamu hizo, Mhe. Mukangara amesema kuwa ni jambo la kusikitisha kumpoteza kiongozi huyo ambaye bado Taifa lilikuwa likimuhitaji hasa katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi Mkuu wa mwezi  Oktoba mwaka huu. 
Waziri huyo ameongeza kuwa Mufti atakumbukwa kwa upole  , unyenyekevu wake na kutopenda makuu,wakati wa uhai wake marehemu alikuwa tayari kumsikiliza kila mtu bila kujali dini au kabila lake. 
“Nimepokea kwa huzuni nyingi taarifa ya kifo cha Sheikh Mkuu wa Tanzania Mufti Shaaban Issa Bin Simba ambaye alikuwa Kiongozi anayeshirikiana vizuri na viongozi wote wa serikali na vyama mbalimbali katika kuhakikisha Watanzania wanaendelea kuwa wamoja” amesema .

Amesema Waziri Mukangara: “Nakutumia salamu zangu za rambirambi wewe Katibu Mkuu, BAKWATA na waislamu wote nchini na naungana nanyi katika kuomboleza msiba huu mkubwa katika nchi yetu. 
Aidha, kupitia BAKWATA, natuma salamu za dhati ya moyo wangu kwa familia ya marehemu kwa kumpoteza mpendwa wao. Napenda wajue kuwa msiba wao ni msiba wangu. Pia, naungana nao katika kumwomba Mwenyezi Mungu, Mwingi wa Rehema aiweke pema peponi roho ya marehemu … Amina.”
Imetolewa na;
Idara ya Habari(MAELEZO)

15 Juni,2015

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 8 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 15, 2015

    Innalilah wainailah Rajiun.

    ReplyDelete
  2. Inna lillahi, waina ilayhi raajiuun. Pole kwa Familiya ya Sheikh wetu, na pole kwetu sote waislam. Allahumma ghfirlahuu, warhamahuu, waskanahuu filjannah! Aamin.

    ReplyDelete
  3. Innalillaahi wa inna ilayhi raajiun....

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 15, 2015

    Yaarab mfanyie nyepesi hesabu yake.
    Yaarab mpe kauli thabit, yaarab lijaalie kaburi lake liwe bustani katika bustani za Peponi.
    AMEEN.

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 15, 2015

    Innaa liLlaahi wa innaa ilayHi raajiuwn.

    May Allaah waive any sins and multiply his reward. Amiyn.

    ReplyDelete
  6. Inna lillahi wa inna ilayhi rajeoun!

    ReplyDelete
  7. Inna lillahi wa inna ilayhi raji'un

    ReplyDelete
  8. Nimeshtushwa na kusikitishwa na taarifa ya kuondoka kwa Mufti Simba. Natoa pole kwa ndugu na marafiki wa marehemu, na wa-Islam. Ni pigo kubwa kwa Taifa. Mimi kama mwalimu nilikuwa ninamwenzi Mufti Simba kama kiongozi aliyekuwa anahamasisha elimu. Niliwahi kuandika hivyo.
    Mungu amweke mahala pema Peponi.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...