Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana (CMSA) imezindua mashindano ya ya insha na kujibu maswali yanayolenga kuelimisha wanafunzi wa vyuo vya elimu ya juu kote nchini kuhusu uelewa wa masoko ya mitaji na dhamana. Mashindano hayo yanayolenga kuongeza ari kwa wanafunzi kujifunza kuhusu masoko ya mitaji yanashindanisha wanafunzi wa vyuo vya elimu ya juu nchini bila kujali taaluma wanayosemea. Uzinduzi rasmi umefanyika tarehe 1 June 2015 mjini Dar es Salaam na yanatarajiwa kumalizika tarehe 15 Julai 2015.

Ushiriki katika mashindano hayo utakua kwa kutuma barua pepe kwa insha na kutuma ujumbe mfupi wa maneno kwa njia ya simu (sms) wenye neno “challenge” kwenda 0766 046 046 halikadhalika kwa kutumia mtandao “google play store” kwa kuandika “CMSA challenge”

Mashindano hayo yatashindanisha wanafunzi wa jinsia ya kike na kiume, hali kadhalika yatahusisha ushindanishi wa vyuo vitakavyotoa washindi wengi zaidi. Zawadi zitakazotolewa ni pamoja na fedha taslimu na safari ya kwenda Afrika ya Kusini kwa wili moja ili kujifunza kwa vitendo kuhusu masoko ya mitaji na dhamana. Kwa taafifa zaidi tembelea tovuti ya CMSA: www.cmsa-tz.org
Picha ya pamoja ya maafisa wa Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana (CMSA), wakiwa pamoja na Afisa Mtendaji Mkuu Bibi Nasama Massinda (wa pili kushoto aliyeketi) na Mwenyekiti wa Chama cha Madalali wa Soko la Hisa la Dar es Salaam Bwana George Fumbuka (wapili kulia aliyeketi) wakati wa hafla ya uzinduzi wa mashindano hayo.
Baadhi ya wanafunzi waliohudhuria uzinduzi wa mashindano ya insha na kujibu maswali ya yanayolenga kuelimisha wanafunzi wa vyuo vya elimu ya juu kote nchini kuhusu uelewa wa masoko ya mitaji na dhamana.
Afisa Mtendaji Mkuu wa CMSA Bibi Nasama Massinda akizundua mashindano ya insha na kujibu maswali ya yanayolenga kuelimisha wanafunzi wa vyuo vya elimu ya juu kote nchini kuhusu uelewa wa masoko ya mitaji na dhamana.
Baadhi ya wanafunzi waliohudhuria uzinduzi wa mashindano ya insha na kujibu maswali ya yanayolenga kuelimisha wanafunzi wa vyuo vya elimu ya juu kote nchini kuhusu uelewa wa masoko ya mitaji na dhamana.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...