ILE Filamu kubwa iliyoshirikisha wasanii mahiri kutoka Tanzania movie Talent Top Ten 2014 (TMT) ipo tayari na inatarajia kuonyeshwa katika jumba la sinema la Mlimani City Cinema Tarehe 12.June. 2015 ni siku ya Ijumaa na itarfuka kwa siku tatu Ijumaa, Jumamosi na Jumapili.
Sinema hiyo ambayo imeshirikisha wasanii wakali wenye elimu ya uigizaji kutoka kwa wakufunzi kutoka Chuo kikuu cha Dar es Salaam imerekodiwa katika viwango vya kimataifa ndio maana inaanza kurushwa katika majumba ya sinema na kuingia sokoni katika Dvd siku ya Jumatatu tarehe 8.June 2015.
Filamu ya Mpango Mbaya ilitengenezwa baada ya shindano la kuibua vipaji kutoka mikoa mbalimbali kumalizika na kubaki na wasanii Bora 10 ambao walipata ofa ya kurekodi sinema hiyo ambayo imekidhi vigezo vya kimataifa ikiwa ni kampeni ya kampuni ya Proin Promotios kujenga mazingira wasanii kufika kimataifa.
Wasanii wanaofanya sinema hiyo kuwa ni ya kipekee ni Mwanaafa Mwinzago mshindi wa milioni 50, Isarito Isaya, Aneth Peter, Tishi Abdalah, Macdolnard Mapunda, Chiki Mchoma, Kaparata Mtawana wasanii wakali kibao wanaofanya vinzuri katika tasnia ya filamu Swahilihood.
Filamu ya Mpango mbaya kutoka kampuni ya Kizalendo ya Proin Promotions Ltd, imetayarishwa na Staford Kihore, na kuongozwa na Muongozaji mahiri wa kimataifa Karabani muandishi wa Muswada ni Novatus Nago Mugurusi ni kazi iliyojaa ujuzi wa kutukuka.
Sinema ya Mpango Mbaya itaingia rasmi katika soko katika mfumo wa Dvd na kusambazwa na kampuni ya usambazaji ya Proin Promotions ya jijini Dar es salaam, ambaye ndio mtayarishaji mkuu, kampuni iliyojitoa kuibuka nyota wapya kutoka popote walipo Tanzania.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...