Wafanya biashara wadogo huamini kwamba kua na tovuti
ni kitu kinachofanywa na wafanya biashara wakubwa na inaitaja gharama nyingi
kutengeneza. Hilo sio kweli. Gharama ya kuwa na website ni ndogo sana
ukilinganisha na faida utakazo zipata baada ya kuwa nayo. Faida ya kuwa na
tovuti ni pamoja na; Biashara yako kuaminika kitaifa na kimataifa. Biashara
zote zilizo halisi na zinazoaminika hua na tovuti. Tovuti yako itasaidia
kuhalalisha biashara yako. Kuwa na tovuti pia itakusaidia kujitangaza kwa bei
rahisi sana kuliko utangazaji wa magazeti, radio, mabango na mwingine wowote. Kwa kuwa tovuti ipo mtandaoni masaa 24 na
mahali popote hivyo basi wateja wako wataweza kukuona mahali popote watakapo
kuwa na kwa muda wowote.
Pamoja na hayo mabadiliko yoyote yatakayo tokea
kwenye biashara yako yanaweza kusambazwa kiurahisi kwa wateja wako. Ukiongeza
bidhaa unazo uza, ukiongeza au ukibadalisha huduma unazozitoa nk. wateja wako
wanapata huu ujumbe kiurahisi bila gharama zozote kwako.
Kutengenezea tovuti ya biashara yako, tumia wasajili
wa tzNIC wenye vibali vinavyokubalika: http://www.tznic.or.tz/index.php/registrars/accredited-registrars.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...