Kaimu Mkurugenzi wa Shirika la Madini la Taifa (STAMICO), Mhandisi Edwin Ngonyani (kushoto mwenye suti ya kijivu) akipata maelezo kutoka kwa mtaalam wa Wizara ya Nishati na Madini, Habas Ngulilapi mara baada ya kuwasili kwenye banda hilo katika Maonesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yanayoendelea katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
Kaimu Mkurugenzi wa Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) Mhandisi Edwin Ngonyani (kushoto) akisaini kitabu cha wageni kwenye banda la Wizara ya Nishati na Madini.
Mtaalam kutoka Kituo cha Jimolojia Tanzania (TGC), Jumanne Shimba ( wa kwanza kulia) akimwonesha Kaimu Mkurugenzi wa Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) Mhandisi Edwin Ngonyani (katikati) moja ya bidhaa zinazotengenezwa na kituo hicho, kwenye banda la Wizara ya Nishati na Madini.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...