Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wananchi wa Biharamulo mjini ikiwa siku ya mwisho ya ziara ya siku 10 mkoani Kagera ambapo alizungumzia changamoto mbali mbali zikiwemo za Bei ya Kahawa, Leseni za Bisahara na Boda Boda, Urahisishwaji wa Biashara mipakani , Katibu Mkuu aliwataka wananchi wa Biharamulo kuacha siasa za kishabiki badala yake kuchagua viongozi wanaofaa na watakaoleta maendeleo.
Katibu Mkuuu wa CCM Abdulrahman Kinana amehitimisha ziara yake hiyo ya kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM na uhai wa Chama katika mkoa wa Kagera kwa mafanikio makubwa.
Katika ziara hiyo Kinana amemaliza ziara hiyo leo Julai 14, 2015, baada ya kutembea jumla ya kilometa 3374, akiwa ametembelea majimbo yote tisa katika wilaya zote nane za mkoa huo.
Ziara hiyo imeonyesha kuwa na mafanikio makubwa kwa kuingiza CCM wanachama wapya 5678 kati ya wanachama 488 wakiwa wamehama kutoka vyama vya upinzani vikiwemo Chadema, CUF na NCCR Mageuzi.
Katika ziara ya mkoa wa Kagera, ambako amesafiri kwa gari nchi kavu na mitumbwi kwenda katika visiwa vitano, amefanya mikutano 74 kati yake ikiwemo mikutano 63 ya hadhara na kuzindua miradi 46, 41 ikiwa ni yamaendeleo ya wananchi.
Wananchi wa Biharamulo mjini wakishangilia jambo kwenye mkutano wa hadhara
Katibu wa Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akihutubia wakazi wa Biharamulo mjini na kuwaambia CCM pekee ndio ina sera zinazotekelezeka na zenye uleta maendeleo kwa wananchi.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Kinana (pichani kulia) akitoka kukagua mradi wa maji wa Nyakahura uliopo wilayani Biharamulo, Mkoa wa Kagera ambao umekwama kutokana na Wizara ya Maji kuwapatia zabuni ya ujenzi wakandarasi wasio faa. Mradi huo unaofadhiriwa na Benki ya Dunia kwa gharama ya sh. bil. 1.4 hadi sasa haujakamilika, jambo linalotia hofu kwamba fedha za mradi huo zimeliwa badala kufanyia kazi iliyokusudiwa.Ndugu Kinana ameamuru wale wote waliohusika kuhujumu mradi huo wasakwe na kuchukuliwa hatua za kisheria.Pichani shoto ni Mkuu wa Mkoa wa Kagera,Mh.Jonh Mongella

Baadhi ya Wananchi wakiwa wameshika mabango yanayolalamikia ufisadi mkubwa uliofanywa katika mradi wa maji wilaya ya Biharamulo.
Mkazi wa kijiji cha Nyakahura Ndugu Majaliwa Issa akiuliza swali kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya Nyakahura Mizani, wilaya ya Biharamulo ambapo alitaka kujua hatua gani zinachukuliwa kwa waliochakachua mradi mkubwa wa maji wilayani humo
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa Nyakahura ambapo aliwaambia wananchi hao waache kuchagua viongozi kwa ushabiki,Katibu Mkuu aliwaeleza wananchi hao kuwa Mbunge wao alipaswa kuwa wa kwanza kufuatilia mradi huo pamoja na madiwani lakini hawakufuatilia,kiasi hata mradi huo kupelekea kupoteza fedha nyingi na wananchi kukosa maji.
Meneja wa Tanesco wilaya ya Biharamulo Ndugu Ernest Miliyango akielezea namna wanavyoendesha shughuli za kuzalisha umeme mara baada ya kupokea mashine mpya ya uzalishaji umeme kwa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwa meambatana na Mganga Mkuu Msaidizi wa kituo cha Afya cha Rutakaragata,Dkt Donasian Kamara,mara baada ya kukagua na kupokea taarifa ya ujenzi wa wodi ya wazazi katika kituo hicho,wiaya ya Biharamulo mkoani Kagera.
PICHA NA MICHUZI JR-BIHARAMULO
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...