Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akielekea kwenye ukumbi wa mkutano wa Sandton Internationa Center unakofanyika mkutano wa wake wa Marais na Wakuu wa Nchi za Afrika huko Johannesburg nchini Afrika Kusini tarehe 15.6.2015. Aliyefuatana na Mama Salma ni Mwenyekiti wa OAFLA anayemaliza muda wake Mama Hinda Derby Itno.
 Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiangalia moja ya machapisho mbalimbali yanayohusiana na Mkutano wa Wake wa Marais na Wakuu wa Nchi za Afrika (OAFLA) unaofanyika nchini Afrika Kusini.
  Wake wa Marais na Wakuu wa Nchi za Afrika wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya ufunguzi wa mkutano wao wa mwaka unaozungumzia uwezeshaji kwa wanawake na Maendeleo katika Bara hili.
 Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akitoa hotuba yake ya mwisho kwenye kikao cha Wake wa Marais na Wakuu wa Nchi za Afrika kinachofanyika kwenye Ukumbi wa Sandton jijini Johannesburg nchini Afrika Kusini tarehe 15.6.2015.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...