Na Hassan Silayo-MAELEZO
Mawakala wa Forodha nchini wameaswa kujisajili katika mfumo wa uondoshaji mizigo wa Himaya moja ya Forodha ya Afrika Mashariki (Single Custom Territory) utakao anza kutumika hivi Karibuni.
Hayo yamesemwa na Kamishna wa Forodha Kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Tiagi Kabisi wakati mkutano na Viongozi na wanachama wa Chama cha Mawakala wa Forodha (TAFA)
Bw. Kabisi alisema kuwa mawakala wa forodha nchini hawana budi kufanya hivyo ili kuwezesha uondoshwaji wa mizigo kwa haraka zaidi pindi mfumo huo utakapoanza kutumika.
“Sasa tunaelekea katika matumizi ya Himaya moja ya Forodha ya Afrika Mashariki yaani Single Custom Territory ili kuwa na uwezo wa kupata huduma kwa kutumia mfumo huo pindi matumizi yatakapoanza mapema ili kuondoa usumbufu utakaoweza kutokea”,alisema Bw. Kabisi
Bw. Kabisi aliongeza kuwa mpaka sasa ni makampuni mawili (2) ya mawakala waliojisajili mpaka sasa, na kwamba mawakala wa forodha hawana budi kuendelea kuwa waamifu ili waendelee kuongoza katika makusanyo ya fedha kwa mwaka ujao ambapo kwa mwaka huu wamechangia kwa asilimia 40 ya mapato ya serikali.
Naye Rais wa Chama cha Mawakala wa Forodha (TAFA) Bw. Stephen Ngatunga alisema kuwa wataendelea kushirikiana na Mamlaka la Mapato Tanzania (TRA) katika kuhakikisha wanaifanya idara ya forodha inafanya vizuri katika makusanyo ya fedha.
Pia Bw. Ngatunga aliitaka serikali kuendelea kushughulikia changamoto mabalimbali zinazoikabili idara hiyo ili kuwawezesha kushiriki kikamilifu na kuendelea kuongoza katika makusanyo ya mapato ya serikali.
Kamishna wa Forodha Kutoka Mamlaka ya
Mapato Tanzania (TRA) Bw. Tiagi Kabisi akiongea na viongozi wa Chama cha
Mawakala wa Forodha na kuwataka mawakala wa Tanzania kujisajili katika mfumo wa
uondoshaji wa Himaya moja ya Forodha(SINGLE CUSTUM TERRITORY) ili kuwezesha uondoshwa
wa mizigo kwa haraka zaidi pindi mfumo
huo utakapoanza kutumika kwani mifumo huo na watanzania tayari zinawasiliana
mpaka sasa, Wakati wa Mkutano uliofanyika leo Jijini Dar es Salaam Kushoto ni
Naibu Kamishna wa Forodha Dkt. Patrick Mugoya
Rais wa Chama cha Mawakala wa Forodha (TAFA)
Bw. Stephen Ngatunga akiongea na
viongozi wa Chama cha Mawakala wa Forodha na wawakilishi wa Mamlaka ya Mapato
Tanzania (TRA) ambapo aliipongeza serikali kupitia Mamlaka hiyo katika
kuhakikisha wanaweka mazingira mazuri kwa mawakala wa forodha na kuiasa
kuendelea kushughulikia changamoto mbalimbali katika sekta hiyo ili kuiwezesha
serikali kupata mapato kwa maendeleo ya Taifa, Wakati wa Mkutano uliofanyika
leo Jijini Dar es Salaam Kulia ni Kamishna wa Forodha Kutoka Mamlaka ya Mapato
Tanzania (TRA) Bw. Tiagi Kabisi.
1- Baadhi
ya wanachama wa Chama cha Mawakala wa Forodha (TAFA) wakichangia wakati wa
mkutano uliokutanisha Viongozi na wanachama wa Chama cha Mawakala wa Forodha
(TAFA) pamoja na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).
Mwanachama wa Chama cha Mawakala wa Forodha (TAFA) akichangia wakati wa
mkutano uliokutanisha Viongozi na wanachama wa Chama cha Mawakala wa Forodha
(TAFA) pamoja na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).
PICHA
NA HASSAN SILAYO-MAELEZO
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...