Na Mwandishi wetu.

Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel Tanzania ikishiriakiana na Huawei
 leo imetangaza kuanza Bazaar lake maalum litakalowawezeha watanzania
kujipatia simu za kisasa za Smart phone na kuweza kufurahia huduma za
zote za intaneti kupitia mtandao wa Airtel

Bazaar la Airtel na Huawei  limepangwa kufanyika kuanzia ijumaa,
jumamosi na jumapili hii kuanzia saa 3asubuhu hadi saa moja usiku
katika eneo la ndani la Mlimani City  na litakuwa na muendelezo
hapohapo na baadae litazunguka katika maeneo mbalimbali nchini.

Akizungumzia Bazaar hilo Meneja masoko wa Airtel Bi Aneth Muga amesema
"Bazaar letu litakuwa la kijanja zaidi kwani simu za smart phone
zitakazouzwa ni bora na zitaambatana na ofa kabambe kuliko zote
zinazopatikana sehemu yoyote".

"Mteja wetu uliopo mahali popote tembelea BAZAAR la Airtel ujinyakulie
simu bora na kisasa kama zile za Huawei au Airtel Red kwa punguzo
kabambe zikiwa na  kifurushi cha intaneti kitakachokupa MB 120, SMS
120 pamoja na muda wa maongezi 120 ofa ambapo huwezi kuipata popote
zaidi ya kweye Airtel Bazaar" alisema Muga

Meneja masoko kutoka Huawei Lyidia Wangari aliongeza kuwa licha ya
simu za Smart phone za Huawei kuuzwa kwa gharama nafuu pia atakaenunua
simu pale atajipatia simu nyingine ya bure au zawadi tofauti tofauti
papo hapo kwa mfano "mteja yeyote kati ya 300 wa kwanza kununua simu
ya Huwawei aina ya Met 7 DUAL atapata simu aina ya Kishkwambi bure
kabisa na atakaenunua simu ya Huawei Met 7 atapata simu ya bure aina
ya Y220 pale pale" alifafanua

Kwa Upande wake Afisa Airte l wa kitengo cha Smartphone Bw, James
Kagashe alisema "tunataka kudhihirisha kwa wateja wetu kuwa Airtel
ndio mtandao sahihi kwa Smartphone yako popote ulipo,   nakuhakikishia
kuwa kila simu inayouzwa katika Artel Bazaar inakuja na ofa kabambe ya
kifurushi cha SMS, dakika za muda wa maongezi pamoja na intanet
itakayokuwezesha kuperuzi upendavyo"

Nawahamasisha wale wote mnaotaka kuenda na wakati kwa kumiliki simu
bora na kuunganishwa na mtandao bora kwa Smartphone yako tembelea
Airtel Bazaar la Airtel Mlimani City  ili tukuunganishe. Alimaliza kwakusema Bw Mwanda.

 Meneja Masoko wa Huwawei Bi Aneth Muga akionyesha kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) simu aina ya Huwawei Met 7 ambayo
zitauzwa katika Airtel Bazaar linalofanyika mlimani City ijumaa,
jumamosi, na jumapili hii ikiwa na ofa ya simu ya bure aina ya
'Huwawei Kishkwambi' iliyoshikiliwa na Meneja Masoko wa Airtel Bi
Aneth Muga. Pia simu hiyo itaunganishwa na ofa kabambe ya kifurushi cha Airtel papo hapo.
 Meneja Masoko wa Airtel Bi Aneth Muga akionyesha kwa wanahabari (hawapo pichani) simu ya kisasa ya Airtel Red itakayopatikana kwa gharama nafuu katika Airtel Bazaar litakalofanyika wiki hii ijumaa,
jumamosi, na jumapili hii pale mlimani City kwa gharama nafuu huku
ikiwa imeunganishwa na kifurushi cha Airtel bure. Anaetazama ni Meneja
Masoko wa Huwawei Bi Lydia Wangari.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...