SHIRIKA la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) limeboresha huduma kwa
wateja wake kwa kubadilisha muonekano wa ofisi zake za jijini Dar es Salaam
ili kupunguza urasimu wa kutoa huduma sanjari na utaratibu wa wateja
kubonyeza kitufe maalum kwaajili ya maoni ya huduma zinazotolewa.
Aidha sekta isiyo rasmi na rasmi zimeaswa kujiunga na mifuko ya
hifadhi ya jamii itakayowawezesha kujikwamua kiuchumi kwani
waliojiandikisha kwenye mifuko ya hifadhi ya jamii ni wachache hali
inayopelekea wazee kujiingiza katika ulinzi .
Hayo yalisemwa na Mkuu wa Idara ya Masoko na Uhusiano wa NSSF, Eunice Chiume wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa
habari jijini Arusha hivi karibuni.
Alisema lengo la kuboresha ofisi hizo ni kuhakikisha wateja wanapata
kile wanachokihitaji sambamba na kuondoa msongamano wa kupata huduma
mbalimbali zinazotolewa na mfuko huo lakini pia wamekuja na huduma
nyingine muhimu kwaajili ya kupima utendaji kazi kwa wafanyakazi
wanaowahudumia wateja.
Alisema sababu nyingine ya kuboresha ofisi za Dar es salaam ni
kutokana na kuwa na wachama wengi ambapo asilimia 75 ya wanachama wa
Mfuko huo wapo huko.
“Lakini tukishamaliza huko tutaenda mikoa mingine kuboresha ofisi na
mazingira ya ofisi yawe mazuri, ili wateja wapate huduma bora na za
uhakika”.
Akizungumzia suala zima la sekta isiyo rasmi na rasmi ni vyema
kujiunga katika mifuko hiyo ya jamii ili waweze kujiwekea akiba na
baadaye kunufaika na mafao mbalimbali kwani vijana hivi sasa
wanafariki na kuwaacha wazee hali inayopelekea wazee kukosa misaada
kwa tegemezi wao na kusababisha kuingia katika sekta mbalimbali ili
waweze kupata fedha za kijikimu na maisha.
“wazee hivi sasa ndio wanabaki na vijana ambao ni tegemezi wanakufa
hivyo ni vyema sasa kuhakikisha watu wanajiunga na mifuko ya hifadhi
za jamii na kuboreshwa maisha yao “.
Mkuu wa Idara ya Masoko na Uhusiano wa NSSF, Eunice Chiume akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati akielezea juu ya Shirika lilivyojipanga kuboresha huduma za wateja wake.
Mkuu wa Idara ya Masoko na Uhusiano wa NSSF, Eunice Chiume akionyesha kifaa maalum cha maoni ya Wateja wa NSSF juu ya huduma wanazozitoa.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...