THE
UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
DIRECTORATE
OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS
Telephone: 255-22-2114512,
2116898
E-mail: ikulucommpress@googlemail.com
Website : www.ikulu.go.tz
Fax: 255-22-2113425 |
PRESIDENT’S OFFICE,
STATE
HOUSE,
1BARACK OBAMA ROAD,
11400
DAR ES SALAAM.
Tanzania.
|
TAARIFA
KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais Jakaya Mrisho Kikwete ametuma
salamu za rambirambi kwa Mkurugenzi wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC),
Bw. Clement Mshana, wafanyakazi wake na waandishi wote kwa ujumla kufuatia kifo
cha mtangazaji na mwandishi mwandamizi wa TBC Bi. Florence Dyauli.
“Pokea rambirambi zangu za dhati kwa
kuondokewa na mwandishi mwandamizi na mahiri Bi. Florence” Rais amesema
“Mbali na uandishi na utangazaji wake
mahiri, Bi. Florence alikua mzalendo wa kweli aliyetumikia taasisi hii ya
serikali kwa uadilifu na upendo wa kweli, tutamkumbuka na tutaukosa mchango
wake. Ni wajibu wetu kumuombea mapumziko mema kwa mwenyezi Mungu na kumshukuru
kwa mchango wake alioutoa kwa moyo wa dhati”. Amesema Rais Kikwete na kuongeza kuwa:
“Hakika Florence tutamkumbuka, nawapa
pole wafanyakazi wote wa TBC na waandishi wote kwa kuondokewa na mwenzao katika
tasnia ya Habari”.
Rais ameongeza.
“Salaam pia ziwafikie ndugu na jamaa wa
Bi. Florence ambao msiba huu ni mkubwa sana kwao na unawagusa sana, naelewa
machungu waliyonayo na huzuni, hata hivyo kwa pamoja ni wakati wa kuzidi
kumuombea Marehemu katika safari yake ya mwisho”. Rais amesema na kuwatakia roho ya
subira na uvumilivu katika kipindi hiki kigumu kwao.
Bi. Florence ambaye amefariki jana 18 Juni, 2015 jijini Dar-es-Salaam alizaliwa
Julai 27, 1961. Bi. Florence alianza kazi katika Radio ya Taifa, Radio Tanzania
Dar-es-Salaam (RTD) na baadaye
Televisheni ya Taifa (TVT) na kwa sasa TBC .
Mwenyezi Mungu ailaze Roho ya Marehemu
mahali pema peponi, Amina.
Imetolewa
na:
Premi Kibanga,
Mwandishi wa Habari wa
Rais, Msaidizi,
Ikulu-DSM
19 Juni, 2015
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...