THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
DIRECTORATE
OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS
Telephone: 255-22-2114512,
2116898
E-mail: ikulucommpress@googlemail.com
Website : www.ikulu.go.tz
Fax: 255-22-2113425 |
|
PRESIDENT’S OFFICE,
STATE
HOUSE,
1 BARACK OBAMA ROAD,
11400
DAR ES SALAAM.
Tanzania.
|
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amepokea
kwa mshutuko na masikitiko taarifa za kifo cha mbunge wa Jimbo la Ukonga, Dar
es Salaam, Mheshimiwa Eugenia Mwaiposya ambaye ameaga dunia usiku wa kuamkia
jana, Jumanne, Juni 2, 2015, mjini Dodoma ambako alikuwa anahudhuria Vikao vya
Bunge.
Katika
salamu zake za rambirambi kwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Mheshimiwa Anna Makinda, Rais Kikwete amesema: “Nimepokea kwa mshutuko na
masikitiko taarifa za kifo cha Mbunge wa Jimbo la Ukonga, Mkoa wa Dar es
Salaam, Mheshimiwa Eugenia Mwaiposya ambaye nimejulishwa ameaga dunia mjini
Dodoma ambako alikuwa anaendelea kuhudhuria Vikao vya Bunge.”
Amesema
Rais Kikwete: “Kwa hakika, taifa letu limepoteza kiongozi muhimu kutokana na kifo
hiki. Mbunge Mwaiposya alikuwa mwakilishi hodari na mtetezi wa kuaminika wa
wananchi wa Jimbo la Ukonga. Napenda kukutumia wewe Mheshimiwa Spika salamu
zangu za rambirambi kwa kupoteza Mbunge mahiri sana. Aidha, kupitia kwako,
nawatumia Wabunge wote salamu zangu za rambirambi kwa kuondokewa na mwenzao.”
Ameongeza
Rais Kikwete: “Kupitia kwako, Mheshimiwa Spika, napenda pia kutuma salamu zangu kwa
wananchi wa Jimbo la Ukonga ambao wamepoteza mwakilishi wao. Mheshimiwa vile
vile, napenda kutoa pole nyingi kwa familia, ndugu na jamaa wa Mbunge Mwaiposya
kwa kuondokewa na mama na mchangiaji mkubwa katika maisha yao. Wajulishe niko
nao katika msiba huu mkubwa. Naelewa uchungu wao katika kipindi hiki na
nawaombea subira ili waweze kuvuka kipindi hiki. Naomboleza nao na naungana nao
katika kumwomba Mwenyezi Mungu aiweke peponi roho ya Mheshimiwa Eugenia
Mwaiposya. Amina.”
Imetolewa
na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya
Rais,
Ikulu,
DAR
ES SALAAM.
2 Juni, 2015
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...