Rais
Mstaafu wa Awamu ya Tatu Mhe. Benjamin William Mkapa atuma salamu za Rambirambi
kwa BAKWATA kufuatia kifo
cha
Mufti Issa Bin Shaaban Simba.
Rais
Mstaafu wa Awamu ya Tatu Mhe. Benjamin Mkapa, amemtumia Kaimu Mufti wa
Tanzania, salamu za rambirambi kufuatia kifo cha Mufti Issa Bin Shaaban Simba
kilichotokea Jumatatu katika hospitali ya TMJ.
Katika
salamu zake Mhe. Mkapa ameelezea kushtushwa kwake na kifo cha Mufti Simba ambae
amemuelea kama kiongozi “aliyekuwa
muadilivu, mpenda amani, mwenye busara na mbobevu mkubwa wa masuala yanayohusu
dini ya kiislamu”. Kwenye salaamu zake Mhe, Mkapa amemuelezea Marehemu
Mufti Simba kuwa alikuwa “kiungo muhimu
sio tu kwa waislamu bali hata kwa serikali na jumuiya za dini mbali mbali”.
Ametoa
pole zake kwa BAKWATA, familia ya Marehemu Mufti Simba, waislamu wote na
watanzania kwa ujumla kwa msiba huu; na amewaombea kwa mungu “awape subira, imani na busara kwenye kipindi
hiki kizito”. Aidha, amewaombea BAKWATA mungu awape “busara na hekima zaidi za kuweza kuendelea kuijenga taasisi hiyo kama
ambavyo Marehemu Mufti Simba alifanya ili iendelee kuwa nguzo muhimu ya amani
na utulivu nchini mwetu” hasa katika kipindi hiki ambapo nchi inapita
katika mitihani kadhaa.
Inna lillahi wa Inna Ilayhi Rajiuun
Imetolewa
na:
Ofisi
ya Rais Mstaafu,
Mhe.
Benjamin William Mkapa.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...