Umesha
jiulizaga kwanini kuna .co, .or, .go, .ac, nakadhalika. Katika Domain Name
System (DNS) yani mfumo wa domain kuna ngazi tofauti. Leo nataka tuongelee SLD
yani Second Level Domain au ngazi ya pili ya domain ambayo hii iko punde tuu
baada ya Top Level Domain (TLD).
Mfano .co
katika .co.tz ni SLD wakati .tz ni TLD (Top Level Domain). Kwa kawaida Second Level Domain (SLD) huwa ina
tambulisha shirika (organization) linalo sajili hio domain liko katika mfumo gani
au ni la aina gani. Kwa hapa Tanzania,
tzNIC wamepanga SLD (Second Level Domain) kama ifutavyo.
- .co.tz – hii ni kwaajili ya kampuni au biashara zilizo sajiliwa kulingana na sheria za usajili wa makampuni ya biashara Tanzania.
- .or.tz – hii ni kwaajili ya mashirika ya sio tafuta faida katika kuendesha shuguli zao.
- .go.tz – hii ni kwaajili ya mashirika ya kiserikali ambayo yame undwa na bunge la Tanzania au yametokana na sera ambazo zimepitishwa na serikali ambayo hufanya kazi ya kuhudumia wananchi kama vile wizara na kadhalika.
- .ac.tz – hii ni kwaajili ya taasisi za elimu ya juu na ufundi.
- .ne.tz – hii ni kwaajili ya makampuni ya mawasliano kwa njia za mtandao.
- .mil.tz – hii ni mahususi kwaajili ya Jeshi la Tanzania na taasisi zinazo husika maswala ya ulinzi.
- .sc.tz – hii ni kwaajili ya shule za awali, msingi pamoja na sekondari.
Hivyo basi kama unataka kuregister domain yako
unatakiwa kuzingatia mfumo huo ili kuwa rahisi kwa wewe kupatikana pale wateja
wako wanapo kutafuta mtandaoni.
Website;
http://www.tznic.or.tz/
Facebook; https://www.facebook.com/tznic
Twitter;
https://twitter.com/tznic
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...