Kibao kinacho elekeza eneo la mradi wa viwanda wilayani Kisarawe mkoani Pwani lililopo Visegese. Mradi huo unaendeshwa na Halmshauri hiyo na wabia wa Kampuni ya World Map
 Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), Brendan Maro (kushoto), akizungumza na viongozi wa Halmshauri ya Wilaya ya Kisarawe,  Wabia wa eneo la mradi wa Kampuni ya World Map  na wawekezaji kutoka nchini China waliofika wilayani humo jana kuangalia fursa za kuwekeza viwanda katika eneo hilo. Kulia ni Ofisa Mipango Miji Mwandamizi kutoka TIC, Elibariki Ngorovily.
 Wawekezaji kutoka China wakiwa katika mkutano na uongozi wa wilaya ya Kisarawe na wabia wa mradi huo kutoka Kampuni ya World Map kabla ya kwenda kuona eneo la mradi wa viwanda. Kutoka kushoto ni Makamu wa Rais wa Umoja wa Makampuni ya Huallan 'Huallan Group', Tu Huobao, Mkurugenzi wa Masoko wa Kampuni hiyo, Apple Ye, Huang Haitao na Meneja Masoko, Nara Zhou.
 Mkurugenzi wa Halmshauri ya Kisarawe, Mwanamvua Mrindoko (kulia), akizungumza katika mkutano huo wakati akiwakaribisha wawekezaji hao. Kutoka kushoto ni Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), Brendan Maro,  Ofisa Mipango Miji Mwandamizi kutoka TIC, Elibariki Ngorovily, Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Subira Kigalu, Mwenyekiti wa Halmshauri hiyo, Adam Ng'imba.

 KWA PICHA ZAIDI BOFYA HAPA.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...