Waziri wa Ujenzi ambaye pia ni Mbunge wa Chato Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli katikati akionyesha kabrasha lenye Fomu ya kuomba kuteuliwa kugombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi CCM mara baada ya kukabidhiwa na Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (Nec) ya CCM wa Idara ya Oganizesheni, Dk. Mohamed Seif Khatibu mkoani Dodoma leo.
Waziri wa Ujenzi ambaye pia ni Mbunge wa Chato Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akisaini kitabu kabla ya kuchukua fomu ya kuomba kuteuliwa kugombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi CCM mkoani Dodoma.
Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (Nec) ya Idara ya Oganizesheni, Dk. Mohamed Seif Khatibu kushoto akimkabidhi fomu Waziri wa Ujenzi Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli.
Waziri wa Ujenzi ambaye pia ni Mbunge wa Chato Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akisoma moja ya fomu aliyokabidhiwa leo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 04, 2015

    Hongera sana Dr. John Magufuri, MUNGU akubariki sana, yakupasa ufunge na kuomba ili BWANA YESU akupe kibali cha kuteuliwa. CCM wakitaka wapate urais kilaini zidi ya UKAWA wanatakiwa wamteue Dr. John Magufuri au Prof. Mark Mwandosya. Si yule kampeni meneja, "chama kwanza urafiki baadae".

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 05, 2015

    Hapa ...hata mie ninaewachukia sanaaaa naweza geuka nyuma na kuangalia vizuri......

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 05, 2015

    COUNT ON MY VOTE!!!!!

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 05, 2015

    Mnaoomba kazi ya kuongoza nchi hii kimya kimya na wale wanaotumia mbwembwe mnakaribishwa kuomba kwa unyenyekevu. Tutachunguza mambi yenu na nia zenu tuchague mwisho wa siku tutachagua mmoja wenu, na kuwashukuru wote waliotangaza nia na kugombea kwa njia mbalimbali. Tunawashukuru kwa kuthubutu, atakayechaguliwa OKtoba tunamatarajio makubwa ya kupiga hatua za maendeleo.

    Eh Mungu tunaomba uchaguzi wa amani usiokuwa na rabsha. Mungu mwenye enzi yote tunaomba pia utupatie kiongozi makini mwenye kuitakia nchi hii mema na maendeleo ya watanzania wote.

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 05, 2015

    Huyu mchapa kazi anaonekana akipewa anaweza kuhamasisha watanzania kuleta maendeleo makubwa.

    ReplyDelete
  6. AnonymousJune 05, 2015

    Tunataka watu kama hawa

    ReplyDelete
  7. AnonymousJune 05, 2015

    Safi sana mzeee

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...