Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel leo imezindua mnara wa mawasiliano katika wilaya ya Ikungi mkoani Singida ambao utasaidia upatikanaji wa mawasiliano na pia kuboresha ubora wa mtandao kwa wakazi wa wilayani hapo na maeneo ya jirani.

Meneja wa kanda ya kati wa Airtel, Bwana Stephen Akyoo, alisema Mnara huo mpya wa mawasilino ni moja kati ya mikakati ya kampuni yake kujitanua zaidi na kuboresha mtandao wa mawasiliano, huku wakiendelea kuangalia namna ya kuendelea kufanya huduma zao kuwa za gharama nafuu na kupatikana kwa wakazi wote nchini. Mnara huo mpya wa mawasiliano utawafaidisha wakazi zaidi ya 15,700 ambao ni wakazi wa wilaya ya ikunga pamoja na vijiji vitano vya jirani vya Mpugizi, Mlandala, Kaugeri, Mduguyu na Kimpuma.

“Tunaamini moja kati ya vikwazo vikubwa vya mawasiliano bora Tanzania ni upatikanaji wa huduma za mawasiliano na ndio dhamira yetu kubwa ya kuhakikisha tunapanua wigo wetu kwa kuzindua minara ya mawasiliano na kuwezesha maeneo yaliyo pembezoni mwa nchi kufikiwa na kupata mawasiliano bora.

Tumekuwa tukitoa kipaombele katika kuboresha upatikanaji wa huduma za mawasiiano katika maeneo ya vijijini tukiamini kwa njia hii tutaweza kuboresha shughuli za kilimo, uvuvi, madini pamoja na shughuli nyingine za kibiashara ambazo ndizo nguzo ya kukua kwa uchumi wan chi yetu. Leo wakazi wa kata ya Mwaru wataweza kunganishwa na mtandao wa kisasa, huduma za kupiga simu pamoja na huduma za Internet nakufurahi huduma zetu nyingi za kibunifu ikiwemo huduma ya Airtel Money.”

Aliongeza kwa kusema ikiwa ni njia ya kuwahudumia wateja wa maeneo haya vyema, Airtel imesajili mawakala zaidi ya watano wa huduma ya Airtel Money katika kijiji cha Mwaru watakaoungana na mawakala wetu zaidi ya 45,000 nchini katika kuhakikisha huduma ya pesa kupitia simu za mkononi inapatikana wakati wote.

Akiongea wakati wa uzinduzi, Diwani wa kata ya Mwaru, Bwana Omary Hassan Mgisa, akimwakilisha Mkuu wa wilaya, aliwapongeza Airtel kwa kuwafikishia mawasiiano kwani hapo awali watu wengi walikuwa na matatizo makubwa ya mawasiliano na kukwamisha shughuli zao kwa kiasi kikubwa. Tunafurahi kwa Airtel kuleta mawasilino haya karibu na watu kwani huduma za mawasiliano ni chachu kubwa katika kukuwa kwa uchumi.”

Napenda kuwashauri wakazi wa hapa kujisajili katika mtandoa wa Airtel nakutumia huduma zao kama vile Airtel Money kufanya miamala ya kifedha kwaajili ya familia zao na biashara zao kwa haraka na usalama zaidi.

“nikiwa kama kiongozi wa eneo hili nahaidi kushirikiana kwa dhati na kuhakikisha makampuni kama Airtel yanayojali wateja wake, wanapata mazingira mazuri ya kuwekeza ili kuendelea kutoa huduma bora na nyingi zaidi kwa jamii” aliongeza Mgisa
Meneja wa kampuni ya Airtell kanda kati bwana Martin Kilasara, akitoa maelezo kwa mgeni rasmi Omary Hassan Mgisa Diwani wa kata ya Mwaru tarafa ya sepuka Wilayani Ikungi Singida Wakati wa Uzinduzi wa Mnara wa Airtel katika kijiji cha mwaru.
Mgeni Rasmi katika uzinduzi wa mnara wa airtelOmar Hassan Mgisa Diwani wa kata ya Mwaru akikata utepe wakati wa uzinduzi wamnara wa airtel katika kijiji cha mwaru wilayani ikungi mkoani Singida jana wakati wa uzinduzi wa mnara huo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...