Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali
Iddi akitoa sadaka kwa Watoto Yatima wa kiumewa Kituo cha Kulelea
Watoto Yatima cha Rahman kiliopo Chang’ombe Mjini Dodoma hapo kwenye
makazi yake Mtaa wa Farahani Mjini Dodoma.Kulia ya Balozi Seif Ali Iddi ni Mkewe Mama Asha Suleiman Iddi.
Balozi Seif Ali Iddi akitoa sadaka kwa Watoto Yatima wa Kike wa Kituo cha Kulelea Watoto Yatima cha Rahman kiliopo Chang’ombe Mjini Dodoma baada ya kufutari nao pamoja.
Baadhi ya Watoto Yatima wa Kituo cha Kulelea Watoto
Yatima cha Rahman kiliopo Chang’ombe Mjini Dodoma wakipata futari ya
pamoja iliyoandaliwa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif
katika Makaazi yake yaliyopo Mtaa wa Farahani Mjini Dodoma.
Picha na – OMR – ZNZ.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi amesisitiza
umuhimu wa Waumini wa Dini ya Kiislamu kuendelea kujenga utamaduni wa
kufutari pamoja ili kudumisha utaratibu uliotiliwa nguvu na Kiongozi
wa Dini hiyo Mtume Muhammad { SAW } na kuendelezwa na maswahaba
waliomfuata.
Balozi Seif ametoa sisitizo hilo kwenye hafla ya Futari ya pamoja
aliyowaandalia Watoto Yatima wanaolelewa katika Kituo cha malezi ya
Watoto yatima cha Kiislamu cha Rahman Kiliopo Chang’ombe Mjini Dodoma.
Futari hiyo ambayo pia ilihudhuriwa na baadhi ya viongozi wa Dini ya
Kiislamu wa Mji wa Dodoma wakiambatana na baadhi ya Viongozi wa
Serikali na Kisiasa ilifanyika katika Makazi yake yaliyopo Mtaa wa
Farahani Mjini Dodoma.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...