Balozi wa Tanzania nchini Oman Mheshimiwa Ali Ahmed Saleh aliandaa hafla ya Futari kwa ajili ya Wawakilishi mbalimbali kutoka serikali ya Oman, Mabalozi, Jumuiya ya wafanya biashara, watanzania na wageni mbalimbali iliyofanyika nyumbani kwa Mheshimiwa Balozi maeneo ya Shatti Al Qurum.
Mgeni rasmi katika Hafla hii alikuwa Sayyid (His Highness) Mohamed bin Salim Al Said , Mkuu wa Itifaki kutoka Wizara ya Mambo ya Nje ya Oman, halfla hii pia ilihudhuriwa na Nasser Al Busaidy, Afisa Mwandamizi katika Idara ya Itifaki ya Ofisi ya Mfalme (Royal Court ) mabaloz mbalimbali akiwemo Balozi wa Afrika Kusini Mheshimiwa Jenerali Chris Pepani, Balozi wa Palestina Ahmed Abbas Ramadhan, Bolozi wa Pakistan Mheshimiwa Ayaz Hussain na Balozi wa Indonesia Mheshimiwa Sukanto pamoja na wawakilishi wa Jumuiya ya wafanya biashara, Marafiki wa Tanzania (Friends of Tanzania) na watanzania wanaoishi Oman.
Wageni waalikwa kinamama wakipata Futari
Mheshimiwa Ali Ahmed Saleh, wa pili kulia Balozi
wa Tanzania nchini Oman akiongea na wageni wake wakati wakipata futari
Wageni waalikwa wakipata Futari
wageni waalikwa wakubwa kwa wadogo wakipata Futari
Waliokaa kutoka kushoto ni Nasser Al Busaidy , Afisa
Mwandamizi katika Idara ya Itifaki ya Ofisi ya Mfalme (Royal Court ) , Mheshimiwa
Ali Ahmed Saleh, Balozi wa Tanzania nchini Oman
katika picha ya pamoja na Mgeni Rasmi His Highness Mohamed bin Salim Al
Said Mheshimwa Chris Pepani, Balozi wa Afrika Kusini na Sheikh Abdallah Al Zakwan, Mwakilishi wa
Jumuiya ya wafanyabiashara
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...