Bodi ya Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania ikiongozwa na Mwenyekiti
wake Bw. Michael Mwanda, imekamilisha ziara ya kukagua miundombinu
ya kuchakata gesi asilia na bomba la gesi asilia katika Mikoa ya Lindi,
Mtwara na Dar es salaam. Katika ziara hiyo Bodi ya TPDC ilipata fursa ya
kujionea na kufanya ukaguzi wa hatua za mwisho za ujenzi wa
miundombinu hiyo.
Moja ya kisima gesi asili kinacho endelea kufanyiwa utafiti, kilichopo kisiwa
cha Songo Songo ambacho kinacho endeshwa na kampuni ya Pan Africa.
Ukaguzi huo umefanyika kwa lengo la kujiridhisha kwamba Mkandarasi
aliyepewa jukumu hilo amelitekeleza kwa umahiri, kulingana na
makubaliano ya mkataba, na zoezi hili linafanyika kabla mkandarasi
hajakabidhi mradi huu kwa TPDC.
Meneja Msimamizi wa Mradi wa bomba la gesi asilia, Bw. Sultani Pwaga, akitoa maelezo kwa Wajumbe wa Bodi juu ya mmomonyoko wa fukwe za bahari katika eneo la Mnazi bay.
Mradi huo umetekelezwa kwa kutumia fedha za mkopo wa masharti nafuu
kutoka Serikali ya Jamhuri ya watu wa China. Jumla ya gharama za ujenzi
wa mradi huu kwa fedha za kigeni ni Dola za Marekani zipatazo bilioni
1.225, ambapo asilimia 95 ni mkopo na asilimia 5 ni mchango wa Serikali.
Ziara Bodi ya Wakurugenzi Shirika ilianza tarehe 25 hadi 29 Julai 2015,
Bodi hiyo ilitembelea eneo la Somanga Fungu kituo cha makutano ya
bomba la gesi kutoka Madimba na Songo Songo, Kiwanda cha kuchakata
gesi asilia Songo Songo, Vituo vya kupokelea gesi asilia Kinyerezi na
Tegeta, pamoja na eneo la Kuchakata gesi asilia Madimba na visima vya
kuzalisha gesi asilia Mnazi bay.
Wajumbe wa Bodi ya TPDC wakipatiwa ufafanuzi katika kituo cha Kinyerezi
jijini Dar es Salaam, katika ziara ya wajumbe wa bodi hiyo kujionea na
kukagua hatua za mwisho za ujenzi wa Miundombinu ya gesi asilia.
Ukaguzi huo umefanyika kwa lengo la kujiridhisha kwamba Mkandarasi
aliyepewa jukumu hilo amelitekeleza kwa umahiri, kulingana na
makubaliano ya mkataba, na zoezi hili linafanyika kabla mkandarasi
hajakabidhi mradi huo kwa TPDC.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...