MAHAKAMA Kuu Kanda ya Dar es Salaam imetupilia mbali kesi
namba 301 iliyofunguliwa na Kampuni ya kufua Umeme ya IPTL, PAP pamoja
na Mkurugenzi wa Kampuni ya PAP Bw Harbinder Singh Sethi dhidi ya Mbunge
wa Kigoma Kusini Mhe David Kafulila kwa madai kuwa Kafulila alichafua
jina kampuni hizo na muhusika huyo kwamba walichota zaidi ya 300bn
kwenye akaunt ya Tegeta escrow kinyume cha sheria na taratibu.
Katika shauri hilo, Kampuni ya IPTL,PAP na Herbinder Singh
Sethi walitaka Mahakama imuamulu Mhe Kafulila alipe fidia ya 310bn kwa
kuchafua jina la kampuni na mkurugenzi huyo.
Katika kesi hiyo Mhe Kafulila alikuwa akitetewa na taasisi
za kisheria za Legal& Human Righ Centre pamoja na kituo cha Human
Righ Deffenders.
Akitoa uamuzi huo mbele ya mawakili wa Human Right
Defenders na Legal & Human Right Center wakiongozwa na wakili
Mtobesya huku mawakili wa IPTL, PAP na Sethi wakiwa hawakufika
mahakamani, Jaji Rosemary Teemba alisema Mahakama Kuu imejiridhisha
kwamba kampuni ya IPTL, PAP na Mkurugenzi wao Harbinder Sethi hawakuwa
na hoja za msingi kuthibitisha madai yao kama msingi wa kufungua kesi
mahakama kuu na hivyo kwa kuzingatia hali hiyo Mahakama Kuu kanda ya Dar
es salaam inatupilia mbali shauri hilo kuanzia.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...