CHAMA cha Wananchi (CUF) wilaya ya Kondoa kimewataka wananchi wa Wilaya hiyo kufanya mageuzi ya uongozi kwa kuchagua wagombea wa vyama vya upinzani ili kuleta mabadiliko ya kiuchumi na kuleta maendeleo.

Hayo yalisemwa na Katibu wa CUF wilaya ya Kondoa, Jafari Ganga alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari Makao Makuu ya CUF Dar es Salaam jana.
Alisema kwa miaka mingi wilaya ya Kondoa imekuwa ikitawaliwa na Chama cha Mapinduzi (CCM)katikangazi mbalimbaliza viongozi wa juu wakiwemo wabunge ambao kila mara wanatoka chama tawala.
Ganga alisema kuendelea kudidimia kwa uchumi wa wilaya hiyo kutokana na uongozi ambao hausimamii ipasavyo maendeleo ya uchumi, hivyo baada ya kuona hivyo CUF ilianza kuonesha njia kwa kusimamia mambo mbalimbali ya kiuchumi yaliyofanya chama kukubalika.
Alisema mpaka sasa katika kata zote 29 za wilaya ya Kondoa zimesimika matawi ya chama hicho na wanatarajia kutwaa viti vya madiwani na Ubunge katika majimbo mawili ya Kondoa Vijijini na Kondoa.
"CUF imeamka inayo matawi 160 katika katika Kata zote 29 za wilaya ya Kondoa, tumejiandaa kutwaa viti vya madiwani na wabunge" alisema Bw. Ganga.
Alizitaja Kata hizo kuwa ni Kondoa mjini, Chemchem, Kilimani, Kingale, Kolo, Bolisa, Serya, Suruke, Hondomairo, Changaa, Thawi, Sowera, Kikilo,Salanka, Bereko, Kisese,Kikore, Itololo,Masange, Mnenia, Itaswi, Bumbuta, Pahi, Kinyasi,Keikei, Busi, Haubi, Kwa Delo, na Kalamba.
Wilaya ya Kondoa umegawanywa na kuwa majimbo mawili ya Kondoa na Kondoa Vijijini pia kuna Jimbo la Chemba ambalo Mbunge wake aliyemaliza muda wake ni Juma Nkamia.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...