Muonekano wa sehemu ya awamu ya kwanza ya Mradi wa Magari Yaendayo Haraka (BRT) ambapo kipindi cha mpito kinatarajia kuanza Septemba mwaka huu. 

Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka (DART) imeisifu serikali ya awamu ya nne chini ya Rais Jakaya Kikwete kwa mafanikio ya ujenzi wa awamu ya kwanza ya Mradi wa Magari Yaendayo Haraka (BRT) ambapo kipindi cha mpito kinatarajia kuanza septemba mwaka huu. 

Mradi huu unatarajia kuboresha maisha ya wakazi wa jiji la Dar es Salaam ambalo limesongwa na msongamano wa magari na kusabisha shughuli mbalimbali kushidwa kupata mafanikio zaidi Mradi huu pia utachoche kasi ya maendeleo katika jiji hili na taifa zima ukizingatia zaidi ya asilimia 80 ya pato la ndani la taifa linachangiwa na jiji la Dar es Salaam. 
Hayo yalisemwa na Mtendaji Mkuu wa DART, Bi, Asteria Mlambo mwishoni mwa juma mara baada ya semina iliyoandaliwa kwa ajili ya waandishi wa habari juu ya mradi huo, kuwa serikali ya awamu ya nne imeweza kufanikisha awamu ya kwanza ya maradi. 
“Sisi watendaji wa DART tunaipongeza serikali ya awamu ya nne ambayo ipo mbioni kumaliza wakati wake,” kwa kuwa imefanyakazi kubwa katika mradi huu aliongeza kusema Bi. Mlambo 
Pia alisema Baraza la Madiwani Halmashauri ya jiji la Dar es Salaam lilikuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha mradi huo unaanza tangu uliporidhiwa na baraza la Mawaziri Julai 6, 2006. 
Maradi huo umeanzishwa na sera ya Taifa ya Usafirishaji ya mwaka 2003 na sera ya Taifa Usafirishaji na Uchukuzi ya mwaka 2001, na upo katika miradi ya serikali ya Mpango Maaalumu wa Matokeo Makubwa sasa (BRN). 
Alifafanua kwamba mradi huo wa BRT ni wa awamu sita; awamu ya kwanza imeghalimiwa na fedha toka benki ya dunia Dola za Kimarekani 325 milioni na serikali ya Tanzania imetumia Tsh. bilioni 23.5. 
Mhandisi wa Wakala wa Mradi wa Mabasi Yaendayo Haraka (DART), John Shauri alisema kipindi cha mpito kipo mbioni kuanza na tayari serikali kupitia wakala wao umetiliana saini ya makubaliano na Kampuni ya UDA Rapid Transit (UDA-RT) kuendesha huduma ya kipindi cha mpito 
“Kwa sasa barabara imekamilika na inaendelea kuwekwa taa za barabarani na kukamilisha vituo,” alisema. 
Aliendelea kusema kuwa kampuni hiyo ya UDA-RT kwa sasa inatarajia kuanza kutoa mafunzo kwa madereva 300 ambao watapata ajira katika mabasi ya mradi huo. 
Kampuni ya UDA Rapid Transit inaundwa na Kampunia ya Usafiri Dar es Salaam UDA na wamiliki wa daladala. Kampuni hiyo inatarajia kuleta mabasi 76 Mwezi Septemba mwaka huu ili kuanza rasmi kipindi cha mpito na mabasi hayo yatakuwa na urefu wa mita 12 na 18 nyenye kubeba abiria 80 na 150.
Mhandisi wa Wakala wa Mradi wa Mabasi Yaendayo Haraka (DART), Bw. John Shauri (kulia) akiwaelekeza waandishi wa habari maendeleo ya vituo vya mradi wa mabasi yaendayo haraka BRT wakati wa ziara kutembelea mradi huo ambapo ilitanguliwa na semina iliyoandaliwa na Wakala huo. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. wajitahidi kufanyia usafi barabara ni CHAFU SANA mpaka aibu hasa pale Jangwani Darajani. wanafagia na kurundika mchanga then hawauzoi unarud tena barabarani kuleta vumbi kwa watumiaji. itunzeni barabara hii jamani ni chafu sana mapaka keroooooooo

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...