Rais Jakaya Mrisho Kikwete, akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa PSPF Bw. Adam Mayingu alipotembelea banda la PSPF katika sherehe za siku ya Magereza zilizofanyika Ukonga jijini Dar es Salaam Mwishoni mwa wiki iliyopita.

·     Wengi wajiuga na Mpango huo
RAIS wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete ameushauri Mfuko wa Pensheni wa PSPF kuendelea kutoa elimu ya Mpango wa uchangiaji wa hiari kwa watanzania.

Mheshimiwa Rais alisema hayo mwishoni mwa wiki iliyopita katika siku ya Magereza alipotembelea banda la PSPF katika maonesho maalum yaliyoandaliwa kwa ajili ya siku hiyo.

Akiwa katika banda la PSPF Mheshimiwa Kikwete alikaribishwa na Mkurugenzi Mkuu wa PSPF Bw. Adam Mayingu ambaye pamoja na mambo mengine alimjulisha juu ya juhudi za PSPF za kuhakikisha kila mtanzania anakuwa katika hifadhi ya jamii kwa kupitia Mpango wa Uchangiaji wa Hiari wa PSPF.

Katika mpango huo mtanzania yeyote aliye katika sekta rasmi na isiyo rasmi anaweza kuwa mwanachama ili mradi awe amefikisha umri wa miaka 18, kiwango cha chini cha kuchangia ni shilingi 10,000 kwa mwezi. Mpango huu ni mkombozi kwa watanzania.

Rais kikwete alifurahishwa na mpango huyo na alimweleza Mkurungezi Mkuu wa PSPF, “Safi sana endeleeni na Mpango huu”.

Mfuko wa Pensheni wa PSPF umeshiriki kwa mafanikio katika siku ya Magereza (Mageraza day) kwa kuweza kutoa elimu ya Mfuko kwa askari wa Jeshi la Magereza na wageni wengine waliohudhuria sherehe hizo ambazo hufanyika kila mwaka kwa lengo la kuonesha huduma mbalimbali zinazotolewa na Jeshi hilo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...