Mmoja wa Wakurugezi wa Kalamu Education Foundation Sis. Kwezi akiongozana na wakurugenzi wenzake kugawa zawadi mbali mbali za Vyakula, Vinywaji, Nguo na Pesa vyenye thamani ya TZS 1,658,000 kwa wagonjwa katika ziara yao ya Kusheherekea Sikukuu ya EID EL-Fitri katika Hospital ya Mwananyamala, Dar es salaam
Mwenyekiti wa Taasisi ya Kalamu Education Foundation, Ndugu Mohamed Kamilagwa akiongozana na Makamu wake Hajjat Asha Mtwangi wakimsikiliza kwa makini mmoja wa Madaktari juu ya Changamoto za wagonjwa wasio na Ndugu na Jinsi Gani Taasisi kama Kalamu Education Foundation inaweza Kusaidiana na Hospitali hiyo kuwasaidia katika kupata tiba kwa urahisi.
Mmoja ya Wakurugenzi wa Taasisi Kalamu Education Wakili Said Abdallah Aziz akiongea na kuwapa matunda wagonjwa Mbali Mbali katika Hospitali ya Mwananyamala katika Shamra Shamra ya Kusheherekea Sikukuu ya EID Fitri.
Mwenyekiti wa Kalamu Education Foundation Ndugu Mohamed Kamilagwa (Mwenye Miwani) alipokuwa akifurahi na watoto wa Kituo Cha watoto Yatima cha Jaribu Orphanage Center Kilichopo Kijiji Cha Jaribu, Wilaya ya Rufiji ambapo Taasisi hiyo alipeleka Vyakula na Vinywaji vyenye thamani ya TZS 650,000 katika kuhakikisha sherehe za EID zinafana kwa watoto hao.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...