Mwenyekiti wa Klabu ya Coastal
Union,Dr.Ahmed Twaha katikati akifuatilia mkutano wake na kamati ndogo
ndogo za klabu hiyo uliofanyika jana,kulia ni Katibu Mkuu wa Coastal
Union,Kassim El Siagi,
Mwenyekiti wa Cpastal Union akiwa katika picha ya pamoja na Kamati ya Mipango na Fedha mara baada ya kumalizika kikao hicho.
………………………………………………………………………….
UONGOZI wa Klabu ya Coastal Union
umeitaka kamati ya ulinzi na usalama kuhakikisha inatimiza wajibu wake
ipasavyo ikiwemo kuhakikisha vitendo vitakavyoweza kuigharimu timu hiyo
wakati wa michuano ya Ligi kuu soka Tanzania bara vinazibitiwa.
Akizungumza mara baada ya
kumalizika kwa kikao baina ya Kamati ndogo ndogo zilizoundwa,Mwenyekiti
wa Klabu ya Coastal Union,Dr.Ahmed Twaha alisema kuwa kumekuwa na
vitendo vingi ambavyo vinajitokeza kwenye michuano ya Ligi kuu Tanzania
bara na kuigharimu timu yetu na kulazimika kulipa faini ambayo ingeweza
kufanya mambo mengine ya maendeleo.
Alisema kutokana na kuwepo kwa
tatizo hilo ndio sababu pekee iliyopelekea kuundwa kamati hiyo ili
kuweza kukabiliana na vitendo vinayoweza kuisababisha hasara ndani ya
klabu hiyo kwani vinakwamisha juhudi za kupiga maendeleo.
“Ukiangalia msimu uliopita
tulipata hasara ya shilingi milioni 3 kwa makosa ya uwanjani na hii
inasababishwa na mashabiki kitendo ambacho kinaharibu sura ya mkoa hivyo
lazima kamati hii italisimamia suala hilo “Alisema Mwenyekiti huyo.
Aidha Mwenyekiti huyo aliitwisha
mzigo mengine kamati ya Nidhamu na Maadili kuhakikisha watu wanaotukana
kwenye mitandaa ya kijamii ikiwemo Facebook, Twiter na mengineyo
watachukuliwa hatua kali za kisheria ili kukomesha vitendo hivyo.
Hata hivyo alisema kuwa kamati
hiyo itakuwa na jukumu kubwa la kuhakikisha ulinzi na usalama
unaimarishwa wakati wa timu hiyo itakapokuwa ikicheza mechi zake kwenye
michuano ya Ligi kuu soka Tanzania bara.
“Lakini pia zamani wapo watu
walikuwa wakitengeneza vitabu vya tiketi na kufanya mapato kuwa madogo
licha ya uwepo wa watu wengi hivyo huu ndio mwisho wao kamati hii pia
itasimamia suala hilo kwani hali hii iliifanya klabu kukosa mapato
“Alisema Mwenyekiti huyo.
Mwenyekiti huyo alisema kuwa
wameweka mipango mizuri ya kuhakikisha timu hiyo inafungua matawi kwenye
mikoa yote timu hiyo itakapokuwa ikienda kushiriki michuano ya Ligi kuu
hapa nchini.
IMETOLEWA NA OFISA HABARI WA COASTAL UNION.
OSCAR ASSENGA.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...