Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotions, Alex Msama akimkabidhi sehemu ya msaada wa vitu mbalimbali kwa mtoto Sophia Said wa kituo cha Yatima cha Maunga cha Kinondoni jijini Dar es Salaam ikiwa ni masandalizi ya Sikukuu ya Idd El Fitr.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotions, Alex Msama akiwakabidhi
sehemu ya msaada wa vitu mbalimbali watoto, Gatson Edward na Bonny Mayanga wa
kituo cha Yatima cha Tuwakomboe cha Temeke jijini Dar es Salaam ikiwa ni
masandalizi ya Sikukuu ya Idd El Fitir. Jumla ya vituo 10 vilinufaika na
msaadahuo ambao umetokana na mapato ya Tamasha la Pasaka la mwaka huu.
Sehemu ya misaada hiyo ikishushwa
KAMPUNI ya Msama Promotions chini ya Mkurugenzi wake Alex Msama, jana iligawa misaada ya vitu mbalimbali vyenye thamani ya shilingi mil 9.5 kwa vituo 10 vya kulea yatima vya jijini Dar es Salaam.
Sehemu ya misaada hiyo ikishushwa
KAMPUNI ya Msama Promotions chini ya Mkurugenzi wake Alex Msama, jana iligawa misaada ya vitu mbalimbali vyenye thamani ya shilingi mil 9.5 kwa vituo 10 vya kulea yatima vya jijini Dar es Salaam.
Akikabidhi misaada
hiyo kwa viongozi na wawakilishi wa vituo hivyo, Msama mwasisi wa
matamasha ya Injili nchini tangu mwaka 2000, alisema ametoa vitu hivyo kuwapa
faraja watoto wa vituo hivyo.
Msama ambaye hivi
karibuni alitoa msaada kama huo wenye thamani
ya shilingi mil 7.5, alisema msaada huo wa jana ni kuwapa faraja watoto hao
kufurahia sikukuu ya Idd el Fitr inayoweza kuangukia kati ya Julai 18 au 19.
“Nimeguswa
kuendelea kusaidia watoto hawa, najisikia faraja na amani ya moyo ninapofanya
hivi nikikumbuka mbali mno, ikiwemo hata maisha niliyowahi kuishi na kuyapitia,
hivyo si kutaka sifa wala umaarufu,” alisema.
Msama ametoa wito kwa
jamii kutambua watoto wanaolelewa katika vituo hivyo si kupenda kwao, bali ni
kutokana na changamoto za kimaisha zilizowapata hadi ku kila mtoto angependa
kulelewa na wazazi wake.
Vituo vilivyopewa
msaada wa vitu mbalimbali kama unga, mchele,
sukari, sabuni na juisi, ni Honoratha, Mwana, Umra, Mujahidina, Zaidi, Hairat,
Sifa, Mwandaliwa na Chakuwama.
Akizungumza baada
ya kupokea msaada huo, Alhaji Mzee ambaye ni mmoja wa watoto wa kituo cha Alhaji
Mzee wa kituo cha Mwandaliwa, alisema ni furaha kubwa kwao kupata msaada huo
kuelekea sikukuu hiyo.
Msama alisema
fedha zilizotumika kununua vitu hivyo ni kutoka katika mfuko wa Tamasha la
Pasaka ambalo hufanyika kila mwaka tangu 2000 chini ya uratibu wa kampuni ya
Msama Promotions.
Msama ni mtu
aliyejipambanua kama mdau mkubwa katika kusaidia jamii kupitia makundi maalumu
kama yatima, walemavu na wajane kwa lengo la kuwapa faraja ya kufurahia maisha kama wengine.
Mbali ya kutoa misaada
mbalimbali kwa makundi hayo kabla au baada ya tamasha la Pasaka kila mwaka,
Msama amewahi kusaidia waathirika wa mabomu ya Gongo la Mboto, mwaka 2011
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...