Kaimu Mkuu wa Biashara TTCL Kanda ya Dar es Salaam, Bw. David Dirisha (wa pili kulia) akiwakabidhi watoto wa Kituo cha watoto yatima cha Mama wa Huruma, kilichopo eneo la Madale Wazo Hill nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam.Kaimu Mkuu wa Biashara TTCL Kanda ya Dar es Salaam, Bw. David Dirisha (wa pili kulia) akiwakabidhi watoto wa Kituo cha watoto yatima cha Mama wa Huruma, kilichopo eneo la Madale Wazo Hill nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam.Baadhi ya wafanyakazi na maofisa wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) wakiimba na kucheza na watoto wa Kituo cha watoto yatima cha Mama wa Huruma, wapopokuwa wakiwakabidhi msaada wa mifuko 70 ya saruji.Baadhi ya wafanyakazi na maofisa wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) wakiimba na kucheza na watoto wa Kituo cha watoto yatima cha Mama wa Huruma, wapopokuwa wakiwakabidhi msaada wa mifuko 70 ya saruji.Kaimu Mkuu wa Biashara TTCL Kanda ya Dar es Salaam, Bw. David Dirisha (wa kwanza kulia walosimama) akizungumza na watoto wa Kituo cha watoto yatima cha Mama wa Huruma, kilichopo eneo la Madale Wazo Hill nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam kabla ya kuwakabidhi msaada wa mifuko 70 ya saruji. Wengine ni wafanyakazi wa TTCL na kituo hicho.Kaimu Mkuu wa Biashara TTCL Kanda ya Dar es Salaam, Bw. David Dirisha (wa kwanza kulia walosimama) akizungumza na watoto wa Kituo cha watoto yatima cha Mama wa Huruma, kilichopo eneo la Madale Wazo Hill nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam kabla ya kuwakabidhi msaada wa mifuko 70 ya saruji. Wengine ni wafanyakazi wa TTCL na kituo hicho.Baadhi ya wafanyakazi na maofisa wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) wakipiga picha ya pamoja na watoto wa Kituo cha watoto yatima cha Mama wa Huruma, pamoja na wasimamizi wa kituo hicho mara baada ya kukabidhi msaada wa mifuko 70 ya saruji.Baadhi ya wafanyakazi na maofisa wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) wakipiga picha ya pamoja na watoto wa Kituo cha watoto yatima cha Mama wa Huruma, pamoja na wasimamizi wa kituo hicho mara baada ya kukabidhi msaada wa mifuko 70 ya saruji.Saruji mifuko 70 ikishushwa kwenye gari mara baada ya kukabidhiwa watoto wa Kituo cha watoto yatima cha Mama wa Huruma na kampuni ya TTCL.Saruji mifuko 70 ikishushwa kwenye gari mara baada ya kukabidhiwa watoto wa Kituo cha watoto yatima cha Mama wa Huruma na kampuni ya TTCL.

KAMPUNI ya Simu Tanzania (TTCL) imetoa msaada wa mifuko ya saruji kwa kituo cha watoto yatima cha Mama wa Huruma, kilichopo eneo la Madale Wazo Hill nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam. Mifuko hiyo 70 ya saruji imekabidhiwa juzi katika kituo hicho na Kaimu Mkuu wa Biashara TTCL Kanda ya Dar es Salaam, Bw. David Dirisha kwa niaba ya Ofisa Mtendaji Mkuu wa kampuni hiyo. 

Akikabidhi msaada huo, Bw. Dirisha alisema kampuni imetoa msaada huo ili kusaidia ujenzi wa kituo cha kulelea watoto yatima na wale wenye mahitaji maalum. Alisema msaada huo waliokabidhi utasaidia kituo hicho kuwa na majengo yake yenyewe kwani kwa sasa wamejihifadhi katika eneo dogo na ambalo sio rafiki sana kwa watoto. Kwa upande wake, Mtawa anayewalea watoto hao, Sr. Christina akipokea msaada huo alisema, anaishukuru kampuni ya TTCL kwa msaada huo; kwani umekuwa chachu ya kuamini kuwa na wao watakuwa na majengo yao na wataweza kusaidia watoto wengi zaidi. 

 Aidha ametoa wito kwa wadau wengine watakao guswa zikiwemo kampuni na taasisi mbalimbali kusaidia kituo hicho ili kiweze kukamilisha kwa wakati  ujenzi wa majengo yake na hatimaye kuhudumia watoto wengi zaidi huku kukiwa na usalama wa kutosha. Hii ni mara ya pili kwa TTCL kukichangia kituo hicho mifuko ya saruji kwani mwaka jana pia ilitoa msaada wa saruji kwa kituo hicho cha watoto yatima cha Mama wa Huruma ambacho kwa sasa kina idadi ya watoto 56 ambapo wavulana ni 26 na wasichana 30.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...