Msimu wa pili wa Kwetu House - “kwetu house, kipaji zaidi ya soka” hili shindano ambalo hujumuisha zaidi wapenzi wa soka wenye Kipaji, jumla ya mikoa mitano (Arusha, Zanzibar, Dodoma, Mbeya na Mwanza) kutoa washiriki zaidi kwa ajili ya kunogesha na kuleta upinzani wa kutosha msimu huu mshindi ataondoka na kitita cha shilingi milioni 15, tofauti na msimu uliopita ambao ilikuwa Sh milioni 10.
Baada ya Kwetu House kusaka Shabiki mwenye Kipaji Kwenye Mikoa ya Arusha, Zanzibar,Dodoma na Mbeya sasa ni zamu ya ROCK CITY *Mwanza kwa Mashabiki wote wa Soka wenye Vipaji tofauti (Mwimbaji,Mchekeshaji,mbunifu wa mavazi,mchoraji n.k) kuonyesha vipaji vyao na hatimye Kupata washiriki watakao iwakilisha Jiji la Mbeya kwenye Jumba la (Kwetu House ) jumla ya washiriki 20 kutoka Mikoa Mitano kukaa kwenye Nyumba ya Kwetu House
Team ya Kwetu House 2015 Msimu wa Pili wakiwa Studio za Jembe FM 93.7 Mwanza Mara Baada ya Mahojiano kuhusiana na KWETU HOUSE 2015 Kwa Jiji la Mwanza.
Mkuu wa Channels Azam TV Madam Stellah Adam akizungumzia KWETU HOUSE 2015 kwa Mwaka huu ambapo Kauli mbiu ni "Kipaji na Soka" Stellah aliongezea Zawadi ya Mshindi wa Mwaka huu imeongezeka kutoka milioni 10 Msimu uliopita Hadi Milioni 15 Kwa Msimu huu wa Pili.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...