Muonekano wa Banda la Mahakama ya Tanzania likiwa katika Viwanja vya Julius Nyerere maarufu kama Viwanja vya Sabasaba, Mahakama ya Tanzania inashiriki katika Maonesho haya lengo likiwa ni kutoa fursa kwa wananchi kupata elimu juu ya taratibu mbalimbali za Mahakama ikiwa ni pamoja na kutoa Malalamiko pamoja na kupokea maoni ya jinsi ya kuboresha huduma ya utoaji haki nchini. Banda la Mahakama lipo mkabala na Banda la Zanzibar ndani ya viwanja vya Sabasaba. Katika Maonesho ya mwaka huu, Mahakama ya Tanzania imepanua wigo wa kutoa huduma zake ambapo katika banda hilo kuna uwakilishi wa kila ngazi ya Mahakama kuanzia Mahakama za Mwanzo, Mahakama za Wilaya/Hakimu Mkazi, Mahakama Kuu pamoja na Divisheni zake ikiwa ni Divisheni ya Ardhi, Biashara na Kazi na Mahakama ya Rufani (T).
Vilevile katika banda hilo pia kuna elimu inatolewa kuhusiana na taratibu mbalimbali za ufunguaji wa kesi za mirathi na kadhalika, wananchi wote wanakaribishwa kutembelea banda hilo. 
 Bi. Wanyenda Kutta, Mkurugenzi Msaidizi wa Utumishi, Mahakama akitoa ufafanuzi wa masuala mbalimbali yahusuyo Mahakama kwa vijana wa scout waliotembelea banda hilo
 Vijana wa scout wakipata maelezo kuhusu mahakama

 Mhe. Eva Nkya, Naibu Msajili Mwandamizi, Mahakama Kuu ya Tanzania akifafanua jambo kwa moja ya wateja waliotembelea banda la Mahakama 
 

Mhe. Frank Mahimbali, Naibu Msajili- Mahakama Kuu Divisheni ya Ardhi akisisitiza jambo kwa wateja waliokuja kupata elimu ya Mahakama.  
Picha na Mary Gwera, Mahakama.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...