Mkurugenzi Mkuu mpya wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Dkt.Ally Yahaya Simba(Kushoto) akisaini kitabu cha wageni baada ya kuwasili ofisini kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bi. Sihaba Nkinga
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bi. Sihaba Nkinga akimueleza Dkt. Ally Yahaya Simba (Kushoto) umuhimu wa kuendelea kufanya kazi kwa pamoja kwa lengo la kukabiliana na changamoto zinazoikabili sekta ya mawasiliano,alipomtembelea leo ofisini kwake.
  Mkurugenzi Mkuu mpya wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Dkt.Ally Yahaya Simba akiongea na Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bi. Sihaba Nkinga na kumhakikishia kufanya kazi kwa pamoja kwa maslahi ya Taifa hasa katika kuiendeleza Sekta ya Mawasiliano Nchini.
 1-    Watendaji wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) wakimsikiliza Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bi. Sihaba Nkinga (mwenye suti nyekundu) alipotembelewa na Mkurugenzi Mkuu mpya wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Dkt.Ally Yahaya Simba (kulia kwa Katibu Mkuu) aliyeteuliwa kushika nafasi ya Prof. John Nkoma aliyemaliza Muda wake.
Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Bw. Assah Mwambene akiwaeleza jambo Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (Hawapo pichani), walipotembelewa na Mkurugenzi Mkuu mpya wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Dkt.Ally Yahaya Simba.Kulia kwake ni Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Habari (MAELEZO) Bw. Raphael Hokororo
 Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Bw. Assah Mwambene akiagana na Mkurugenzi Mkuu mpya wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Dkt.Ally Yahaya Simba(kushoto) Picha na Hassan Silayo-MAELEZO

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...