Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na
Teknolojia, Profesa Makame Mbarawa hivi karibuni alimteua Dk. Ally Yahaya Simba (pichani) kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya
Mawasiliano Tanzania, (TCRA) kufuatia mchakato wa kumpata Mkurugenzi Mkuu kama ilivyoainishwa
katika Sheria ya Kuanzishwa kwa Mamlaka ya Mawasiliano ya 2003 kifungu cha 9 na
kifungu cha 13. (TCRA Act, 2003).
Dk. Simba aliteuliwa rasmi kushika wadhifa
huo mnamo tarehe 6 Jula1 2015 kwa kipindi cha miaka mitano. Kabla ya uteuzi
huo, Dk. Simba alikuwa Kaimu Mkurugenzi wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano
(TEHAMA) Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia tangu Agosti 2013.
Dk.
Simba ana uzoefu wa zaidi ya miaka 16 katika Sekta ya Mawasiliano ambapo
amefanya kazi kwa watoa huduma, Taaluma ya Utafiti, Udhibiti pamoja na Serikali
Kuu.
Dk. Simba ana Shahada ya B.Sc. (Hons.) Shahada
ya Sayansi ya Elektroniki na Mawasiliano kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam,
Tanzania, aliyopata mwaka 1998. Pia ana Shahada ya Uzamili ya Uhandisi
aliyoipata mwaka 2003 na Shahada ya Uzamivu (Ph.D) ya Uhandisi wa Kielektroniki
kutoka Chuo Kikuu cha Hokkaido, Sapporo, nchini Japan, aliyoipata mwaka 2006.
Kuanzia
mwaka 2006 mpaka 2011, alikuwa Mtaalamu Mtafiti katika Taasisi ya Taifa ya
Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (NICT), huko Tokyo, Japan, ambako alihusika
katika kufanya utafiti wa madhara ya ya kiafya kwa mwanadamu kwa kutumia simu
za mikononi na kwa kuwa karibu na minara ya mawasiliano.
Mnamo mwaka 2011 hadi mwaka 2013, alifanya
kazi Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kama Meneja Mipango na Utafiti wa
Mamlaka.
Dk. Simba ametoa machapisho kadhaa katika
majarida ya kimataifa na amewasilisha matokeo ya tafiti zake katika zaidi ya
mikutano Zaidi ya 30 ya kimataifa. Aidha Dk. Simba alikuwa Kiongozi wa Timu ya
wataalamu wa Kitanzania iliyoandaa Sheria za Uhalifu wa Mitandao nchini
iliyopitishwa na Bunge hivi karibuni.
Dk. Simba ni Mhandishi Mahiri (Chartered Engineer), aliyesajiliwa
nchini Uingereza katika Baraza la
Uhandisi nchini humo na ni “Fellow” wa Taasisi ya Uhandisi na Teknolojia ya nchini
Uingereza (IET), ambako alikuwa Mshauri wa Kimataifa wa Usajili wa Wanataaluma Wahandisi kutoka
Aprili 2011 mpaka Machi 2014. Pia Dk. Simba ni Mwanachama Mwandamizi wa “Institute
of Electrical and Electronics Engineers” (IEEE). Hali kadhalika Dk. Simba amechapishwa
katika jarida la “Marquis Who's Who in
Science and Engineering” katika toleo la 11, la mwaka 2011–2012.
Dr. Simba ni miongoni waliopata Udhamini wa
Serikali ya Japan (Monbusho Scholarship) kutoka mwaka 2000 mpaka 2006.
Hongeta mwenyekiti wangu!..
ReplyDeleteHakika nakumbuka vema umakini wako ukiwa hapa., Kazi njema.
Kaka michu. Nawe hongera kwa mbunge mtarajiwa hahahaha.
Mdau jp.
Uzoefu wa kazi inaonekana bado kwenye CV yake. Ila Elimu imekaa vizuri. Hongera sana!!
ReplyDelete