Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mh. Said Meck Sadick akizindua kampeni ya kuosha Magari katika viwanja vya Leaders Club kwa ajili ya kuchangia Fedha kwa waandishi wa habari ambao wanamatatizo ya Kiafya ikiwemo Saratani ( MEDIA CAR WASH FOR CANCER).
Mkurugenzi
wa Idara ya Habari (MAELEZO), BW. Assah Mwambene (kulia) akikabidhi kiasi cha
fedha kwa Mmoja wa Waratibu wa MEDIA CAR WASH FOR CANCER Bw. Benjamin
Thomson, zilizochangwa na Idara hiyo kupitia chama chao cha Maofisa
Habari wa Serikali ambao walichanga kiasi cha shilingi
Milioni 1,680,000=. Katikati ni Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mhe. Paul Makonda.
Wizara ya
Habari,Vijana,Utamaduni na michezo pia imechangia shilingi 1,350,000/= baada ya kuguswa na kampeni hiyo adhimu ya kuwachangia waandishi wa Habari wenye Matatizo mbalimbali yakiwemo ya Saratani.
Kampeni hiyo imefanyika leo katika viwanja vya Leaders Club Kinondoni jijini Dar es salaam ambapo viongozi
mbalimbali wakiwemo na wadau wa habari walishiriki zoezi la kuosha
magari kwa kuchangia kiasi chochote cha fedha, Mgeni rasmi akiwa
Mkuu wa Mkoa Dar Es Salaam Mhe. Said Meck Sadick.
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mhe. Paul Makonda akishiriki kuosha moja ya Magari yaliyofika kuoshwa katika MEDIA CAR WASH FOR CANCER kuchangia waandishi wa habari wenye magonjwa mbalimbali ikiwemo Saratani.
Kiongozi Mkuu wa Chama cha ACT Wazalendo Zitto Kabwe akiosha Gari wakati wa Shughuli hiyo maalum kwa ajili ya Kuchangia waandishi wenye udhoofu wa afya zao (MEDIA CAR WASH FOR CANCER).
Ankali akiosha Moja ya Magari kwa ajili ya kuchangia waandishi wa habari ambao wana maradhi mbalimbali ikiwa ni pamoja na Saratani
Mkurugenzi wa Idara ya Habari MAELEZO Bw. Assah Mwambene akimshukuru Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mhe. Paul Makonda mara baada ya kushiriki zoezi la kuwachangia waandishi wa Habari wenye Matatizo mbalimbali yakiwemo ya Saratani (MEDIA CAR WASH FOR CANCER).
Picha ya pamoja ya waandishi wa
Habari pamoja na Baadhi ya Viongozi.
Unaweza Changia pia kupitia M-Pesa 0766 970240
au Tigo Pesa 0653 155 808.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...