Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Mh. Chiku Gallawa akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani), juu ya uwepo wa Mikutano Mikubwa ya Chama cha Mapinduzi katika Mkoa wake, inayotarajiwa kuanza rasmi kesho Julai 8, 2015, yenye agenda kuu ya kuchagua mgombea wa Urais atakaiwakilisha CCM kwenye Uchaguzi Mkuu wa mwezi Oktoba mwaka huu. Katika taarifa yake aliyoitoa leo Julai 7, 2015 Ofisini kwake, Mh. Gallawa amesema kuwa Mikutano hiyo itahusisha uwepo wa wageni wengi Mkoani Dodoma, hivyo kama Mkoa wamejipanga vyema kuwapokea wageni hao na kuwahudumia huku akiwatoa hofu kwa kuwahakikishia hali ya usalama kuwa ni ya uhakika. pia amewataka wale wote ambao hawahusiki na Mkutano huo na wala sio waalikwa, kutofika kabisa Mkoani Dodoma kwa sasa.
Sehemu ya Wanahabari kutoka vyombo mbalimbali wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Mh. Chiku Gallawa wakati akizungumza nao juu ya uwepo wa Mikutano Mikubwa ya Chama cha Mapinduzi katika Mkoa wake.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...