Mwandishi wa habari na mtangazaji maarufu nchini Abdallah Idrissa Majura (pichani) jana ameahidi kufanya mapinduzi ya michezo katika jimbo la kawe ambao utakuwa ni mfano kwa maeneo mengine na taifa kwa ujumla.
Akizungumza na vyombo vya habari mara baada ya kurejesha fomu za kuomba kugombea ubunge jimbo la kawe kupitia chama cha mapinduzi, amesema endapo atapendekezwa na ccm kisha kuchaguliwa kuwa munge wa jimb hilo ataanza na michezo mitano ambayo ni soka, mpira wa kikapu,netiboli, wavu na mpira wa mikono.
"Mungu akinijaalia nikatimiza ndoto yangu ya miaka mingi nitaanza na michezo hii ambapo tutaunda timu moja yenye wachezaji mahiri katika kila mchezo na zote zitajulikana kwa jina moja tu kawe united"alisema mtangazaji huyo ambaye pia ni mwanamichezo maarufu.
Amesema amekuwa akishangazwa kuona michezo kama mpira wa kikapu, netiboli, wavu na mpira wa mikono haipigi hatua wakati haina gharama kubwa za uendeshaji kulinganisha na soka ambayolicha ya kuhitaji fedha nyingi pia kuna ubabaishaji mkubwa ambapo viongozi wengi wanaougoza mchezo nia ni kupata manufaa binafsi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...