Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye akizungumza na waandishi wa habari usiku huu nje ya ukumbi wa White House, Makao Makuu ya CCM Mjini Dodoma, mara baada ya kumalizika kwa Kikao cha Kamati Kuu ya CCM, kilichokaa kupitisha majina matano ya wagombea Urais yatakayopelekwa kwenye Mkutano wa Halmashauri Kuu ya CCM kujadiliawa hapo saa nne asubuhi. Nape hakutaja majina ya wagomea hao waliopita kwenye tano bora, kwa kuseka atataja asuhuhi. 
Muda mfupi baada ya Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye, kumaliza kuzungumza na waandishi wa habari, walitoka wajumbe watatu wa Kamati Kuu ambao ni Dkt. Emmanuel Nchimbi, Mh. Sophia Simba na Mh. Adam Kimbisa ambao walizungumza na waandishi wa habari juu ya walichokizungumza kwenye kikao hicho, ambapo wao walisema wamegomea makubaliano ya majina yaliyopitishwa kwenye kikao hicho kwa madai kwamba Kikao kikekiuka tararibu za uchujaji wa majina hayo. kwani yalijadiliwa majina machache tu na kupitishwa kwenda tano bora, lakini nao hawakuyataja majina hayo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 11, 2015

    Wacha picha iendelee

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 11, 2015

    Ni Membe, Magufuli, Migiro, Januari Makamba na Amina s Ali. Migiro ndio atashinda na Tanzania itapata rais wa kwanza Mwanamke mchapa kazi!

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 11, 2015

    Tunashukuru kwa taarifa na picha.
    Lakini mbona mwanasiasa maarufu sanA na mzee mwenye busara nyingi sana - KINGUNGE NGOMBALE MWIRU sijamuona kwenye picha yoyote? Au ana udhuru?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...